Barnaba: Sijutii kwa niliekuwa nae
Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa
kizazi kipya nchini, Barnaba Elias ‘Barnaba’ ameachia kibao chake kipya
kinachokwenda kwa jina la ‘Sijutii kwa niliekuwa nae’.
Akizungumza jijini Dar
es Salaam, Barnaba alisema wimbo huo kaupeleka sokoni wiki iliyopita na
kwamba imeshaanza kufanya vizuri katika soko hilo, kitu ambacho kinampa moyo wa
kufanya kazi hiyo.
“Kama kawaida yangu
nyimbo zangu nyingi huwa haziwachukizi mashabiki wangu ni jambo ambalo
namshukuru mungu kwani ni wasanii wachache ambao nyimbo zao zinafanya vizuri
mtaani,” alisema.
Barnaba alisema
anawaomba mashabiki wa muziki huo kuendelea kumpa sapoti katika kazi zake ikiwa
ni pamoja na kukaa mkao wa kula kwaajili ya kuzipokea kazi nyingine.
Mbali na kibao hicho,
Barnaba alishawahi tamba na vibao vyake kama, Magubegube, Wrong number,
Tulizana, Milele daima na nyinginezo ambazo zinafanya vizuri katika tasnia ya
muziki wa kizazi kipya nchini.
You might also like:
Post a Comment