Baadhi ya
Wachezaji wa Samsal Mikocheji wakishangilia na Kikombe pamoja na hundi ya
shilingi milioni moja mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya Soka
la ufukweni yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika ufukwe wa Coco Beach jijini
Dar es Salaam.
|
Baadhi ya
Wachezaji wa Samsal wakimpongeza Kocha wao kwa kumrusha juu mara baada ya
kuibuka mabingwa katika mashindano ya Soka la ufukweni yaliyomalizika mwishoni
mwa wiki katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.Timu hiyo ilizawadiwa
Kikombe na hundi ya shilingi milioni moja.
Na Mwandishi
wetu.
TIMU ya
Samsal yenye makazi yake Mikocheni jijini Dar es Salaam wameibuka mabingwa
katika mashindino ya Soka la ufukweni lililomalizika mwishoni mwa wiki na hivyo
kuzawadia kikombe pamoja na hundi ya Shilingi milioni moja.
Samsal
waliibuka mabingwa baada ya kuifunga timu ya Safina yenye makazi yake Ukonga
jijini Dar es Salaam 3-2, na kwa matokeo hayo nafasi ya pili ilichukuliwa na
timu ya Safina na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi laki sita(600,000/=).
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Verge Africa, Rajan Kumar ambao ndio
waratibu alisema mashindano haya yalianza na Kampeni ya kufanya usafi Ufukwe wa
Coco Beach kwa kushirikisha Wafanyakazu wa makampuni ya Pepsi, RedBull, Slipway
Hoteli, G1 Security Limited, AfyaPal(Muhimbili),Toshiba, Zenufa, Hasafa
Science, Verge Africa na Nipe Fagio juni 15,2019 na baadae pakafuatiwa
mashindano ya soka la ufukweni ambalo limemalizika mwishoni mwa wiki hii kwa
kushirikisha timu 14 ambazo ni Dar
Beach Warmer, Every Living things, Safina Athletics, Mkude Fc, Osterbay City,
JMK Fc, Beach Boys, CBE Combine, Samsal Fc, All Stars, We Kick Balls Fc, GEGE
Fc, Gerezani Fc, Future Stars.
Kumar aliyashukuru makampuni yote yaliyojitokeza kushiriki Kampeni hiyo
pamoja na timu shiriki zote na kuwaomba wasikose kujitokeza tena mwakani.
|
Post a Comment