ad

ad

Makampuni yaungana kufanya usafi Coco Beach.

 Baadhi ya wafanyakazi kutoka makampuni mbalimbali ya jijini Dar es Salaam wakishangilia kwa kutiana hamasa mara baada ya kufanya usafi katika ufukwe wa Coco Beach ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa usafi Baharini na kuunga mkono Kampeni ya Serikali ya kutokomeza matumizi ya mifuko ya plastiki iliyofanyika leo Coco Beach jijini Dar es Salaam.Makampuni yaliyojitokeza kufanya usafi ni Pepsi, RedBull, Slipway Hoteli, G1 Security Limited, AfyaPal(Muhimbili), Verge Africa, Toshiba, Zenufa, Hasafa Science na Nipe Fagio.
 Baadhi ya wafanyakazi kutoka makampuni mbalimbali ya jijini Dar es Salaam wakifanya usafi katika ufukwe wa Coco Beach ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa usafi Baharini na kuunga mkono Kampeni ya Serikali ya kutokomeza matumizi ya mifuko ya plastiki iliyofanyika leo Coco Beach jijini Dar es Salaam.Makampuni yaliyojitokeza kufanya usafi ni Pepsi, RedBull, Slipway Hoteli, G1 Security Limited, AfyaPal(Muhimbili), Verge Africa, Toshiba ,  Zenufa, Hasafa Science Nipe Fagio.
 Baadhi ya wafanyakazi kutoka makampuni mbalimbali ya jijini Dar es Salaam wakiwa na mifuko ya uchafu mara baada ya kufanya usafi katika ufukwe wa Coco Beach ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa usafi Baharini na kuunga mkono Kampeni ya Serikali ya kutokomeza matumizi ya mifuko ya plastiki iliyofanyika leo Coco Beach jijini Dar es Salaam.Makampuni yaliyojitokeza kufanya usafi ni Pepsi, RedBull, Slipway Hoteli, G1 Security Limited, AfyaPal(Muhimbili), Verge  Africa, Toshiba,  Zenufa, Hasafa Science na Nipe Fagio. 


Na Mwandishi Wetu.
BAADHI ya Makampuni mbalimbali jijini Dar es Salaam yaungana kufanya usafi ufukwe wa Coco Beach katika kuadhimisha mwezi wa usafi Baharini ambapo huadhimishwa Juni 8 kila mwaka pamoja na kuunga mkono Kampeni ya Serikali ya matumizi ya mifuko ya Plastiki.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwakilishi wa waratibu wa shughuli hiyo kutoka Kampuni ya Verge  Africa, Hafsa Mambosasa alisema wao kwa kushirikiana na makampuni rafiki wameungana kufanya shughuli hii ya kijamii ikiwa ni sehema ya kuihamasisha jamii kuwa swala la kutunza mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu.
Mratibu Hafsa aliyataja makampuni yaliyojitokeza kuwa ni Kampuni ya vinywaji ya Pepsi, Red Bull, Hoteli ya Slipway, G1 Security Limited, AfyaPal(Muhimbili),Verge Africa, Toshiba,  Zenufa, Hasafa Science na Nipe Fagio.
Shughuli za usafi hizo zitafauatiwa na mashindano ya mpira wa miguu wa ufukweni kwa kushilikisha timu mbalimbli za jijini Dar es Salaam ambapo tamati yake inatarajiwa kuwa juni 23,2019 na bingwa atajinyakulia kitita cha pesa taslimu Shilingi milioni moja, mshindi wa pili shilingi laki sita na watatu watapata Vocha ya kulala katika Hoteli ya Slipway.

No comments