ad

ad

Four Ways mabingwa Castle Africa 5 aside Bonanza.

 Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli(kushoto) akimkabidhi Kikombe nahodha wa timu ya Four Ways Park Fc ya Kinondoni, Vidian Samson mara baada ya kuibuka mabingwa katika finali za Bonanza la Castle Africa 5s lililofanyika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu.
TIMU Four Ways Fark Fc yenye makazi yake Kinondoni jijini Dar es Salaam wameibuka mabingwa katika Bonanza kubwa la Soka  lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Posta Kijitonyama kwa udhamini wa Kampuni ya Bia nchini (TBL) kupitia bia yake ya Castle Lager na hivyo kuzawadiwa Kikombe, Medali za dhahabu, Pesa taslimu shilingi 1,500,000/=, Caton ya bia ya Castle Lager pamoja na kuwakilisha nchi katika fainali za Caslte Africa 5s zinazotarajiwa kufanyika mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo.
Four Ways Park Fc waliutwaa ubingwa kwa point 7 wakifuatiwa na Jacks Pub Fckwa pont 4 ambao walizawadiwa Medali za Silva, Catoni ya bia ya Castle Lager na pesa taslimu Shilingi 900,000/=
Mshindi wa tatu ni katika fainali hizo ni Meeda Night Club Fc ambao walipata pointi 3 na hivyo kuzawadiwa medali feddha, Caton ya bia ya Castle Lager pamoja na pesa taslimu Shilingi 600,000/=
Akizungumza na wachezaji, waandishi wa habari pamoja na wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye Bonanza hilo, Menager Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli alianza kwa kuwapongeza mabingwa Four Ways Park Fc kwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo ikiwa ni mara ya pili sasa kufanyika kwa Tanzania  na akawaomba zawadi walizopata zikawe chachu ya maandalizi bora ya fainali za Castle Afica 5s ambazo zinatarajiwa kufanyika nchini Tanzania.
Kikuli pia aliwapongeza timu ya pili nay a tatu kwa ushindi na akato pongezi kwa timu shiriki zote kwa kujitoa kwao katika fainali hizo na kwa jinsi hiyo wakajiandae kwa mashindano mengine mwakani.
 Pamela aliutaja mchakato ulivyokuwa wa kuzipata timu ambao ulianzia kwenye Baa 60 za jijini Dar es Salaam ambapo Bar zilishindana kwa kununua Bia za Castle Lager na kukusanya vizipo na mwisho tukapata timu 32 zilizoongoza na ndizo zimeweza kushiriki Bonanza mpaka kumpata Bingwa ambaye ni Four Ways Park Fc.
Nae Balozi wa Bia ya Castle Africa 5s Tanzania, Ivo Mapunda aliishukuru Kampuni ya Bia Nchini(TBL) kwa uratibu mzuri wa mashindano ya Castle Africa 5s mwaka huu kwani yamekuwa na hamasa ya hali ya juu na kuwaomba waendelee kudhamini mashindano hayo kwani kupitia Bonanza hili wapo waliopata marafiki na mambo mengine mengi kwa sababu ya Bonanza hili kupitia Bia ya Castle Lager ambayo imetuunganisha pamoja.

Baadhi ya wachezaji na mashabiki wa timu ya Four Ways Park Fc wakishangilia na kikombe mara baada ya kuibuka mabingwa katika finali za Bonanza la Castle Africa 5s lililofanyika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam 

No comments