IZO ZILIPENDWA YA MATONYA VIDEONI
Na Elizabeth John
BAADA ya kufanya vizuri na wimbo wake wa ‘Taxi
bubu’, Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Seif Shaban ‘Matonya’, ameachia
video ya kibao chake cha ‘Izo Zilipendwa’ kinachofanya vizuri katika vituo
mbalimbali vya redio.
Akizungumza jijini Dar es Salaama
jana, Matonya alisema anamshukuru Mungu kibao chake kufanya vizuri kwani ni
dalili nzuri ya kazi zake kukubalika, hivyo kuwaahidi wapenzi na mashabiki wake
mambo mazuri zaidi.
“Kiukweli kazi hii imefanya vizuri, kitu ambacho
kinanipa matumaini katika ‘game’ na natumaini video hii itakuwa bora zaidi,”
alisema Matonya.
Matonya amewasihi mashabiki wake kukaa mkao wa kula
kukisubiri kibao hicho na kwamba yuko katika hatua za mwisho za uandaaji wa
kibao hicho.
Mbali ya kibao hicho, Matonya amewahi kutamba na
vibao mbalimbali mahiri kama ‘Anita’,
‘Vaileth’ na vinginevyo ambavyo vilimtambulisha kwa wapenzi na mashabiki
wa muziki wa kizazi kipya.
Post a Comment