Afande Sele anaukaribisha mwaka mpya
Na
Elizabeth John
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Seleman Msindi
‘Afande Sele’ anajipanga kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Soma
Ule’ ambayo itakua ngoma ya kuukaribisha mwaka 2013.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,
Afande Sele alisema wimbo huo utakua ujumbe wa kufungia mwaka na kuukaribisha
mwaka mpya na kwamba yupo katika hatua za mwisho za uaandaaji wa kibao hicho.
“Audio nishamaliza saivi nafanya video, unajua redio saivi
hazina soko sana watu wengi wanapenda kuangalia na sio kusikiliza, hivyo
namalizia kurekodi video baada ya hapo ntaipelela sokoni, kikubwa ni sapoti
kutoka kwa mashabiki,” alisema Afande Sele.
Mbali na hilo, Afande Sele alisema kwasasa wanaendelea na
mchakato wa kusaidia jamii kwa kutoa fedha pamoja na vifaa vya hospitalini kama
shukrani kwa wadau wa kazi zao, ambapo unaongozwa na mkali wa muziki huo, Joseph
Haule ‘Professa Jay’.
Post a Comment