MCHAKATO WA AWALI WA KUPATA TIMUA 32 ZA KUSHIRIKI MASHINDANO YA SOKA YA MSIMU WA PILI YA ‘CASTLE LAGER 5s ASIDE KUKAMILIA WIKI HII, JIJINI DAR ES SALAAM.
Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli. |
KAMPUNI ya Bia
Tanzania(TBL) kupitaa bia yake ya Castle Lager kwa mara nyingine tena imekuja
na mashindano ya “Castle Lager 5s Aside”(wachezaji watano watano kila upande)
msimu wa pili jijini Dar es Salaam utakaoshirikisha takribani Bar 60 za jiji la
Dar es Salam.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli alisema tayari
mchakato wa kutafuta timu shiriki za fainali za mashindano hayo kupitia timu za
promosheni kwenye Bar mbalimbali za jijini Dar es Salaam umeshaanza na tayari
Bar 48 tumeshazifikiwa ambapo wiki hii tunatarajia kuzifikia tena Bar 12 kukamilisha
Bar 60 kwa raundi ya kwanza.
Tutarudi tena
kwa raundi ya pili katika hizo Bar kuhakiki timu zao na Bar 32 zitakazokuwa
zimeongoza kwa mauzo zitakuwa zimefuzu rasmi kuingia kwenye fainali ya Bonanza kubwa
litakayofanyika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam alisema Kikuli.
Aidha Kikuli aliwashukuru
wakazi wa jijini Dar es Salaam kwa kuitikia wito kwani mwamko wa mwaka huu ni
mkubwa ukilinganisha na mwaka jana kwa wakazi wa jijini Dar es Salaam, kwani
kila Bar miongoni mwa Bar 60 zilizoingia kwenye mchakato zinashauku ya kutaka
kushiriki mashindano hayo.
Mashindano haya yanafanyika
hapa nchini kwa mara ya pili, chini ya udhamini wa Bia ya Castle Lager. Hata
hivyo yamekuwa yakifanyika katika nchi nyingine za Afrika.
Mwaka jana tuliyafanya
kwa mara ya kwanza na kupata mwakilishi aliyeshiriki katika michuano ya Kimataifa
ya Afrika, iliyofanyika nchini Zambia kwa kuzikutanisha timu za Afrika Kusini,
Zimbabwe, Swaziland Lesotho na wenyeji Zambia.
Mwaka huu, tunatarajia
kuwa na mashindano bora zaidi yatakayotusaidia kupata washindani na mabalozi
wazuri katika michuano ya kimataifa.
Mchakato wa
kupata timu zitakazoshiriki katika bonanza hilo umeboreshwa zaidi mwaka huu, ambapo
washiriki watapatikana kupitia katika promosheni zitakazofanyika katika baa mbalimbali
jijini Dar es Salaam.
Lengo ni kuwafikia
wanywaji wa bia ya Castle Lager ikiwa ni pamoja na kuwapa fursa ya kutimiza
ndoto zao.
Timu zetu za
promosheni zimekuwa zikipita baa mbalimbalia kwaajili ya kutoa maelekezo kwa
wateja kwa namna ambayo wanaweza kushiriki katika uundaji wa timu zao.
Ili kuingia 32
bora, moja ya kigezo muhimu ni kufanya mauzo mengi ambapo kutakuwa na makasha
maalumu katika baa husika kwaajili ya kukusanyia vizibo baada ya mteja kununua
bia ya Castle Lager.
Niwaombe
watanzania kutumia nafasi hii, ambayo itawapa wakati mzuri wa kutimiza ndoto
zao. Wakati mwingine fursa kama hizi ni nadra sana kutokea.
Castle Lager
tunaendelea kuwapa kile kilicho bora wateja wetu, ikiwa ni pamoja na kusaidia
shughuli mbalimbali za kijamii ikiwamo kukuza na kutoa fursa kwa wenye vipaji
vya michezo.
Mwisho, Nirudie kusisitiza kwamba, michuano
ya Castle Lager 5- Aside ina nafasi kubwa ya kuitangaza nchi yetu, na kutangaza
vipaji binafsi kwasababu inafanyika hadi ngazi ya kimataifa.
Post a Comment