Darling yazindua mtindo mpya wa nywele
Wanamitindo
kutoka Kampuni ya Shahbaaz wakionyesha mitindo mbalimbali ya matumizi nywele
wakati wa uzinduzi wa nywele za zambarau(purple) kutoka Kampuni ya Darling
uliofanyika katika Ukumbi wa King Solomoni Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mwanamziki wa nyimbo za kizazi kipya, Maua Samma akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa nywele za zambarau kutoka Kampuni ya Darling uliofanyika jana katika Ukumbi wa King Solomoni Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Ukiwa
na lengo la kuboresha urembo na kuleta mabadilko ya mwanamke wa Africa kupitia
mitindo kadhaa ya nywele, mtindo mpya umebuniwa kwa rangi mbili;nyekundu na
zambarau na rangi zenye mvuto zaidi.
Darling
ni miongoni mwa vinara wa mitindo mbalimbali ya nywele Tanzania wakishirikiana
na Kaneka Makers of Kanekalon Quality Fibers. Mwaka 2011, Godrej Consumer
Products Ltd iliingia makubaliano na Darling Group. Kwa kutumia uwezo wa pande
zote mbili walijenga umaarufu wa bidhaa na kuongeza uwezo wa usambazaji.
Kwa
sasa, Darling inafanya kazi katika nchi 21 Africa. Kampuni hii ina uzoefu wa
zaidi ya miaka 30 kwenye soko la biashara ya mitindo ya nywele. Hii ina maana
ya kwamba Darling ina furaha kuwa kinara katika nchi hizo za Africa ambapo
inaendesha biashara yake.
Kutokana
na mitindo mbalimbali ya nywele na bei nafuu, ubunifu na uzoefu, Bidhaa ya Darling
inatumiwa na zaidi ya wanawake milioni 150 katika Bara la Africa.
Nchini
Tanzania, mbali na kuwa na bidhaa tofauti, kampuni hiyo imezindua mitindo
mingine mitatu mipya tofauti ya nywele; Kuna Coco Curls, ambayo inalainisha
katika mguso wenye urembo ambao unadumu
kwa muda mrefu kuliko Crotchet nyingine katika soko. Kuna mwonekano laini wa
nywele ambao unaweza kutengenezwa kuwa laini kabisa tofauti na ilivyo kawaida
au kama Crotchet na Afro Baby, ambapo hivi vyote vinachangia mwonekano wa
nywele asilia duniani kote.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha Biashara Africa na Afrika ya Kati, Chirag Savla, alisema “Darling inatambua kwamba, mwaname wa kisasa anataka mengi zaidi kutoka
nje ya maisha yake na ukombozi katika mitindo tofauti ya nywele. Tuna kiu juu
ya kuleta mabadiliko katika nywele ambayo yanaweza kuwa na nguvu kwa fikra ya
mwanamke. Darling inampa bidhaa bora mwanake wa Africa na uhuru wa kutochoka
kuchagua mtindo wowote wa nywele wakati wotewote kwa wepesi. Tunatoa mitindo yenye
ubunifu wa nywele inayokwenda sambamba na thamani ya pesa.”
“Kukidhi
mahitaji yao, mara nyingi tunawasaidia wanawake katika kipindi cha mpito kuwa
na chaguo bora katika mfululizo wa mwonekano. Darling kwa sasa inaendesha kampeni maalumu ya
‘FindYourBeautiful’. Hii ni kampeni
ambayo inamuwezesha mwanamke wa Afrika kufikia malengo yake kwa kile
kinachomfanya kuwa mrembo zaidi, kujiamini, kuwa kama yeye,kwenda na mabadiliko
kwa kuzingatia wajibu wake, kubadilika kimawazo au hata mabadiliko ya akipendacho.”
Alisema Meneja wa Sigma Hair Ind LTD,
Manish Kumar.
Darling
inaamini kwamba kila mwanamke wa Kiafrika lazime awe mzuri jinsi anavyotakiwa. Kuonekana
zaidi kama mbunifu wa kimitindo, wakati akishiriki majukumu mbalimbali kuyafanya
kuwa rahisi na yenye mafanikio kwa mwanamke wa kila siku.
Katika
kuboresha soko lake, Darling ina salon nzuri na za kuvutia pamoja na kiwanda
jijini Dar es Salaam. Darling wanajali
maoni kutoka kwa wateja wao wanaotumia
bidhaa zao mara kwa mara.
Post a Comment