ad

ad

Uzinduzi wa Jukwaa la Mawasiliano ya Afya Kwa Watu Wazima



Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Esther Mariki (kulia) akizindua Jukwaa la NAWEZA litakalolenga mawasiliano ya Afya kwa Watu Wazima na Watoto lililozinduliwa jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Mratibu wa Afya ya Uzazi Wizara ya Afya, Martha Shakinyau, Mkurugenzi wa Mawasiliano USAID Tulonge Afya, Prisca Rwezahura na Dokta Jaiws Hiliza.
SERIKALI ili kupunguza vifo vya uzazi Mama na Mtoto ikishirikiana na Mradi wa USAID Tulonge Afya fhi 360  imezindua Jukwaa la mawasiliano ya afya kwa watu wazima (NAWEZA) ili kufikisha elimu sahihi itakayoijengea jamii ya Watanzania uwezo na kubadilisha mitizamo na tabia zao za kiafya na kuleta matokeo chanya.
Pia jukwaa hilo unganishi litatoa huduma jumuishi za afya katika maeneo matano ya afya kuiwezesha serikali kufanikisha mikakati na vipaumbele vyake vya kupunguza maambukizi ya Ukimwi (VVU), vifo vya  akina mama vitokanavyo na uzazi,vifo vya watoto wachanga, malaria na kifua kikuu (TB).
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa USAID Tulonge Afya, Prisca Rwezahura (kulia) akizungumzajambo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la NAWEZA lenye malengo ya mawasiliano ya Kiafra kwa Watu Wazima na Watoto lililozinduliwa jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo jana Mratibu wa Afya ya Uzazi Wizara ya Afya,Martha Shakinyau alisema NAWEZA itaunganisha jitihada za wadau wa miradi ya mawasiliano ya kuhamasisha na kutoa elimu na maarifa sahihi kwa jamii,  familia, makundi rika ili kubadilisha tabia kulingana na mahitaji na vipaumbele vya maisha yao wakati wa ujauzito au wa malezi ya watoto chini ya umri wa miaka mitano , kuwapa ari ya kuboresha afya zao na kuishi maisha bora.Mratibu wa Afya ya Uzazi Wizara ya Afya, Martha Shakinyau, Akiwasilisha maada wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la NAWEZA lenye malengo ya mawasiliano ya Kiafra kwa Watu Wazima na Watoto lililozinduliwa jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Baadghi ya Wadau wa Afya kutoka sehemu mbalimbali jijini Mwanza wakifuatili kwa makini utambulisho wa Jukwaa la NAWEZA LENYE Malengo ya mawasiliano ya Afya kwa Watu Wazima na Watoto.
“Serikali imejitahidi kuboresha huduma kwa kujenga vituo vya afya,upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na vitedanishi ili kupunguza vifo vya Mama vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga chini ya miaka mitano lakini vifo hivyo vimeendelea kutokea kutokana na changamoto mbalimbali,”
“NAWEZA inalenga maeneo matano muhimu ya vipaumbele vya serikali vya kupunguza maambukizi ya VVU, malaria, afya ya uzazi kabla na baada ya kujifungua,afya ya mama na mtoto na TB.Tunaamini Watanzania wote wakiguswa kwenye eneo moja la kiafya kati ya yaliyoanishwa afya za wengi zitaboreka,”alisema Shakinyau.
Hivyo, NAWEZA itawafikia wananchi tofauti tofauti itachangia kuboresha afya na ustawi wa Watanania wengi, itakuwa ikibadilika badilika ili kukidhi mahitaji ya maeneo mengine ya kiafya muhimu kwa walengwa hao ama makundi mengine.
Kwa mujibu wa Shakinyau changamoto ya umbali wa vituo, umaskini, ukosefu wa elimu ya uzazi salama kwa jamii, huduma za afya zisizokidhi, mila na desturi potofu, uhaba wa dawa, huduma hafifu za rufaa,watoa huduma wa kada zisizo rasmi wasio na weledi, ushirikishaji mdogo wa wanaume na jamii, viongozi wa dini, wanasiasa na serikali.
“Asilimia kubwa ya vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga vinazuilika endapo wadau wa maendeleo, serikali na jamii itawekeza kwa pamoja katika ubunifu na kudhibiti vifo,kuongeza kasi ya uwajibikaji kwenye ngazi zote za utoaji huduma.Pia,ili kufikia Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati, kila mmoja ana jukumu la kuikumbusha jamii kuweza kupunguza vifo hivyo.
“Rais  John Magufuli anataka kuipeleka Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ili kufikia huko, kipimo ni kupungua kwa vifo vinavyotokana na uzazi usio salama na watoto wachanga.Tunatamani  kuvipunguza vifo vya akina mama kutoka 556hadi 292 kati ya vizazi hai 100,000na watoto kutoka vifo 25 hadi 16 kati ya 1,000 kwa mwaka ifikapo 2020,”alisema Shakinyau.
Aidha kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Esther Mariki akizindua jukwaa hilo alisema Kanda ya Ziwa ina changamoto nyingi kutokana na kuwa na idadi kubwa ya vifo vya wajawazito na watoto wachanga huku maambukizi ya VVU yakiwa juu.
Hivyo serikali kuwekeza kwenye sekta ya afya ina imani NAWEZA katika kuboresha na kuhamasisha jamii na wajawazito kuhudhuria kliniki na vituo vya kutolea huduma baada ya kupata ujauzito kutapunguza vifo na pia  kutaibua wateja wapya wa maambuki ya VVU.
Pia malezi ya watoto chini ya miaka mitano yanayozingatia maadili pamoja na mila na desturi yataleta mabadiliko chanya kwenye jamii na katika kuhakikisha kunakuwa na ujauzito salama na wanajifungua salama akinamama wahudhurie kliniki kabla ya ujauzito kutimiza wiki 12 na wakamilishe mahudhurio manane kliniki wakati wa ujauzito.
Aidha, kaimu mganga mkuu huyo alihimiza watumie IPTP ili kumkinga mtoto na madhara yanatokanayo na malaria, kumkinga kwa chandarua chenye dawa, kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya,kunyonyesha ndani ya saa moja baada ya kujifungua, kuzungumza na mtoa huduma na kupeleka watoto kliniki baada ya kutimiza wiki nne hadi sita kwenda kituo cha kutoa huduma wanapoona dalili za hatari.

No comments