WASANII WA KIKE WA KIAFRIKA WAIMBAJI WA MUZIKI WA HIP HOP WAUNGANA KUSHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE
WAKATI dunia
ikijiandaa kutoa heshima kwa wanawake duniani kote katika Siku ya Kimataifa ya
Wanawake Duniani, chapa ya bia ya kibunifu zaidi Africa, Castle Lite, imeanza
safari ya kusherehekea wanawake katika bara zima kwa kuwezesha ushirikiano
mkubwa uliopata kutokea wa wasanii wa kike katika muziki wa Hip-Hop kwenye
ardhi mama. Lengo lilikuwa ni kuonyesha nguvu pale wanawake wanaposimama pamoja
na kuimarisha umoja kwa kupitia muziki, hivyo chapa yetu ilishirikiana na
kikundi cha wasanii wakubwa watano (5) wa muziki wa kufoka na kutengeneza tena
nyimbo ya msanii malkia wa Hip Hop Queen Latifah iliyokuwa maarufu katika miaka
ya 90 ya, U.N.I.T.Y.
Afrika ya Kusini, Tanzania na
Nigeria kwa pamoja waliungana kutengeneza wimbo huu, huku wasanii kama Moozlie
(South Africa), Gigi Lamayne (Afrika ya Kusini), Rouge (Afrika ya Kusini),
Rossa Ree (Tanzania) na Mz Kizz (Nigeria) wakiwa nyuma ya kipaza sauti.
U.N.I.T.Y kutoka Castle Lite ni zaidi tu ya “wimbo mwingine unaoshirikisha
wasanii wa kike wa Hip-Hop”, ni wimbo wa kusherekea na wito, sio tu kwa
wanawake wote barani kote bali katika kila sehemu ya dunia, kuweka uhai katika
nguvu ya wanawake katika muungano.
Wasanii watano kwa wakati mmoja
waliimba U.N.I.T.Y mubashara asubuhi ya leo katika Instagram; Jambo la kwanza
kabisa kufanyika kwa Castle Lite na kwa bara zima la Afrika kwa ujumla.
Akizungumza baada ya onyesho (livestream),
Mkurugenzi wa chapa ya Castle Lite Silke Bucker alisema: “Msingi wetu kama
Castle Lite kila siku umekuwa ni kuvuka mipaka kwa kutumia ubunifu, na ili
kuweka kumbukumbu katika siku hii ya kipekee, hakukuwa na njia nzuri zaidi
kwetu kuunganisha wanawake zaidi bali kwa kutumia jambo ambalo kiukweli
tunalolipenda – muziki.”
“Mshikamano wa kimuziki katika bara zima ulifanya
jambo hili la wasanii kuja pamoja kufanya wimbo pamoja na chapa yetu kuwa la
asili, na Castle Lite imebahatika imeamua kuwaweka wanawake katika hip-hop
mbele. Leo sote tunasherekea nguvu ya wanawake katika UMOJA na
1
tunazidi kung’ara zaidi na kwa fahari kubwa tukisherekea na wanawake wote duniani
kote katika siku hii ya kipekee na ya kimataifa,” Bucker alimalizia kusema.
“Ni hesima kubwa sana kuwa sehemu ya harakati ambazo sio tu kwamba
zinasherekea na wanawake, lakini zinachochea
UMOJA kwa kupitia muziki. Muziki
una uwezo wa kuunganisha watu kutoka katika mazingira tofauti, na ni kwa
kupitia suala hili tuliweza kufanya jambo la tofauti kwa namna yetu ya kipekee ili
kutengeneza wimbo huu mzuri ukiwa na ujumbe wenye nguvu.” Moozlie Aliongeza
Mwaka jana, chapa hii yenye bia
ya baridi ilivunja mipaka ya kimuziki ilipokuwa mwenyeji wa onyesho la kwanza
na la kipekee la wasanii wa kike wa Hip Hop lililoitwa Hip Hop Herstory, ambalo lilijikita katika kuonyesha nafasi ya
wanawake katika mabadiliko ya Hip Hop. Onyesho la Hip Hop Herstory kutoka
Castle Lite lilifanikiwa na baada ya kujifunza kutokana na hilo ilimaanisha
kwamba ushirikiano wa U.N.I.T.Y sio tu kwamba ulikuwa na mantiki lakini pia ni
hatua kwenda mbele katika kuonyesha na kutoa heshima kwa vipaji na michango ya
wasanii wetu wenyewe kutoka Afrika.
Kwa taarifa zaidi fuata kurasa
zetu rasmi katika mitandao ya kijamii:
Facebook : @CastleLite
Twitter: @CastleLiteSA
Instagram: @CastleLiteSA
______________________________________________________________________________
Imesambazwa
kwa niaba ya Castle Lite na Idara ya Masoko na Mawasiliano ya M-Sports
Kwa
mawasiliano zaidi na maombi ya mahojiano tafadhali wasiliana nasi kupitia:
(011) 781-9721
Post a Comment