METROPOLITAN TANZANIA YATIMIZA MIAKA KUMI YA HUDUMA KWA WATANZANIA
Waziri wa
Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa sherehe fupi ya miaka kumi ya Metropolitan iliyofanyika katika
Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Waziri wa
Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza na wageni
waalikwa wakati wa sherehe fupi ya miaka kumi ya Metropolitan iliyofanyika
katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Metropolitan Tanzania,
Aman Mboma akizungumza na wandishi wa habari wakati wa sherehe fupi ya miaka
kumi ya Metropolitan iliyofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya
wageni waalikwa waliohudhuria hafla fupi ya miaka kumi ya Metropolitan wakimsikiliza
Waziri wa Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage(hayupo pichani).
KAMPUNI ya Metropolitan Tanzania ilianzishwa
kutokana na Kampuni ya Metropolitan International ambayo inamilikiwa na MMI
Holdings.
Nchini Tanzania, Kampuni hii inayojihusisha na
masuala ya Bima ilianza huduma zake rasmi Juni 7, 2016 ikiwa chini ya Kapuni ya
Momentum Tanzania (PTY) Limited.
Leo hii Metropolitan Tanzania inaadhimisha
miaka kumi yenye mafanikio katika utoaji wa huduma zake nchini, huku ikitangaza
kuboresha huduma zake zaidi katika utoaji wa huduma za bima.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam, katika hafla maalumu, Mkurugenzi Mtendaji wa Metropolitan
Tanzania….. alisema kuwa miaka mitatu baada ya kuanzishwa kwa kapuni hiyo,
walijikuta wakiwa katika orodha ya kampuni bora na zinazokua kwa haraka katika
soko la bima nchini
“Tangu kupewa jina la Metropolitan Tanzania lililotokana
na muungano wa Momentum and Metropolitan in 2013, kampuni hii imekuwa katika
soko la bima nchini tangu wakati huo ikifanya vyema na ofisi zake zikiwa jijini
Dar es Salaam,” alisema
Aliongeza kusema “Hivi karibuni kampuni ya MMI
ikiwa kama mwekezaji wa kigeni nchini imewekeza jumla ya mtaji wa shilingi za kitanzania bilioni 7.4. lakini kabla ya
hapo Desemba 2105 mtaji wa kampuni hiyo ulikuwa shilingi za kitanzania bilioni
8.5”.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, jumla ya mtaji
wa kampuni hiyo hadi sasa ni shilingi za kitanzania bilioni 16, hali ambayo
inaifanya kampuni hiyo kuwa miongoni mwa kampuni zinazofanya vizuri katika soko
la bima kwa kuwa na msimamo mzuri wa mtaji.
“Kampuni hii inapoadhimisha miaka kumi ya
huduma zake nchini, niwafamishe wadau wetu wote kuwa tunaahidi kuendelea kutoa
huduma bora na kujiimarisha zaidi kibiashara ili tuendelee kuwapo katika soko
kwa mafanikio”.
Post a Comment