Deogratius Mboya bingwa wa kuchesha Dar.
Meneja Mauzo
na Usambazaji Kinywaji cha Valeur kutoka Kampuni ya TDL, Mwesigwa Mchuruza(kushoto)
akimkabidhi Hundi ya Shilingi Milioni mbili mshindi wa shindano la kuchekeza
lililojulikana kama “Valeur Comedy Nights 2016”, Deogratias Mboya mara baada ya
kutangazwa, shindano hilo lilifanyiaka mwishoni mwa wiki katika Bar ya Forty
Forty Tabata jijini Dar es Salaam.Wapili kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa
Kampuni ya Vuvuzela iliyokuwa ikiendesha shindano hilo, Evans Bukuku na Afisa
Sanaa na Burudani kutoka Basata, Augustino Makame.
Mshindi wa
shindano la kuchekesha lililojulikana kama “Valeur Comedy Nights 2016”,
Deogratias Mboya(katikati) akifurahi na kitita cha pesa taslimu Shilingi
milioni mbili mara baada ya kukabidhiwa kama mshindi wa shidano hilo 2016
lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Bar ya Forty Forty Tabata jijini Dar es
Salaam.Kutoka kulia ni Afisa Sanaa na Burudani kutoka Basata, Augustino Makame,
Meneja Mauzo na Usambazaji Kinywaji cha Valeur kutoka Kampuni ya TDL, Mwesigwa
Mchuruza na Mchuruza na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Vuvuzela iliyokuwa
ikiendesha shindano hilo, Evans Bukuku.
Deogratius
Mboya bingwa wa kuchesha Dar.
Na Mwandishi
Wetu.
Deogratius
Mboya amejinyakulia ubingwa wa kuchekesha katika shindano lililomalizika
mwishoni mwa wiki chini ya udhamini wa kinywaji cha Valeur lililojulikana kama
‘Valeur Comedy Nights 2016” na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi milioni
mbili(2,000 000/-),Tuzo maalum ya ushindi na mafunzo kwa videndo na kampuni ya
Vuvuzela kwa muda wa miezi sita.
Nafasi ya
pili ilichukuliwa na Hamphley Richard ambaye alizawadiwa Tuzo maalumu ya
mshindi wa pili pamoja na mafunzo kwa videndo na kampuni ya Vuvuzela kwa muda
wa miezi sita na nafasi ya tatu ni Adam Mbweche ambaye pia alizawadiwa tuzo
maalum ya ushindi wa nafasi ya tatu pamoja na mafunzo kwa videndo na kampuni ya
Vuvuzela kwa muda wa miezi sita.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mgeni raasmi Afisa Sanaa na Burudani kutoka Basata,
Augustino Makame aliwapongeza Kampuni ya Vuvuzela kwa kuendesha shindano hilo
katika kiwango cha hali ya juu lakini pia kwa hamasa ya wakazi wa jiji la Dar
es Salaam waliohudhuria shindano hilo hii inaonyesha dhahili watu wanaelewa
sasa Sanaa ya uchekeshaji.
Makame
alimaliza kwa kutoa wito kwa Kampuni ya Vuvuzela kutanua uwigo sasa wa kufikira
kwenda kisaka vipaji pia na mikoani.
Nae Meneja
Mauzo na Usambazaji Kinywaji cha Valeur kutoka Kampuni ya TDL, Mwesigwa
Mchuruza alimpongeza mshindi kwa kujinyakulia kitita cha Shilingi Milioni mbili
na kumuomba akaitumie vizuri kwani ni pesa ndogo kwa starehe lakini ni pesa
nyingi sana kama akiifanya kama mtaji wa ujasiliamali unaweza kumtoa hapo
alipo.
Mchuruza
aliwapongeza pia washiriki wote kwa kufika hatua ya fainali lakini mwisho wa
siku lazima apatikane mshindi mmoja lakini pia aliwapongeza kwa kuja na
mashabiki wao kwani wamelifanya shindano kuwa lenye hamasa ya hali ya juu ukilinganisha
na mwaka jana.
Washiriki
waliofanikiwa kuingia fainali walikuwa kumi na nane(18) kutoka vitongoji
mbalimbali vya Mkoa wa Dar es Salaam.
Post a Comment