Topland Mabingwa Nane nane Pool.
Baadhi ya
Mashabiki na wachezaji wa Pool wa Klabu ya Topland yenye makazi yake Magomeni
Kinondoni wakiwa wamembeba Nahodha wa
klabu akiwa na kikombe mara baada ya kibuka mabingwa katika fainali za
mashindano ya Pool ya siku kuu ya Nane nane yaliyojulikana kwa “88” Pool
Competitions 2016, yaliyo malizika juzi wakati wa siku kuu hiyo katika Viwanja
vya Bashnet Mtongani jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya
Mashabiki na wachezaji wa Pool wa Klabu ya Topland yenye makazi yake Magomeni
Kinondoni wakishangila na kikombe mara
baada ya kibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Pool ya siku kuu ya
Nane nane yaliyojulikana kwa “88” Pool Competitions 2016, yaliyo malizika juzi
wakati wa siku kuu hiyo katika Viwanja vya Bashnet Mtongani jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa chama cha Pool Taifa(TAPA), Isaach Togocho(kulia) akimkabidhi kikimbe
nahodha wa klabu ya Topland ya Magomeni Kinondoni, Patrick Nyangusi mara baada
ya ya kibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Pool ya siku kuu ya Nane
nane yaliyojulikana kwa “88” Pool Competitions 2016, yaliyo malizika juzi
wakati wa siku kuu hiyo katika Viwanja vya Bashnet Mtongani jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti
wa chama cha Pool Taifa(TAPA), Isaach Togocho(kulia) akimkabidhi pesa taslimu
Shilingi laki tano nahodha wa klabu ya Topland ya Magomeni Kinondoni, Patrick
Nyangusi mara baada ya kibuka mabingwa
katika fainali za mashindano ya Pool ya siku kuu ya Nane nane yaliyojulikana
kwa “88” Pool Competitions 2016, yaliyo malizika juzi wakati wa siku kuu hiyo
katika Viwanja vya Bashnet Mtongani jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mwenyekiti
wa Chama cha Pool Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni, Mathayo Makemba.
Bingwa wa Singles, Issa Selemani akikabidhiwa zawadi yake.
Na Mwandishi Wetu.
TIMU ya Topland yenye makazi yake Magomeni, Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni jijini Dar es Salaam wameibuka mabingwa katika mashindano ya mchezo wa Pool yajulikanayo kama “88” Pool Competitions 2016 baada ya kuwafunga timu ya Dodoma 13 – 4, na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi laki tano (500,000/=) na Kikombe.
Topland walitwaa ubingwa
huo katika mashindano hayo yaliyoshirikisha Vilabu 16 vya mchezo wa Pool kutoka
mikoa mbali mbali.
Nafasi ya pili ilichukuliwa
na Dodoma ambao walizawadiwa pesa taslimu Shilingi laki mbili na
nusu(250,000).Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Klabu ya Fuoni kutoka Zanzibar
ambao walishinda kwa kuwafunga klabu ya
Sunset 13 – 5 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu shilingi laki moja na
nusu(150,000) na nasafi ya nne ilichukuliwa na Sunset ambao walizawadiwa kifuta
jasho cha Shilingi elfu hamsini(50,000).
Upande wa mchezaji mmoja
mmoja (Singles), mchezaji Issa Selemani kutoka Klabu ya Mpo Afrika Ilala
aliibuka kuwa bingwa baada ya kumfunga Hussein Madroback kutoka Klabu ya
Kayumba ya Mkoa wa kimichezo ya Ilala 5 – 3, na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu
Shilingi laki mbili (200,000) pamoja na ngao.
Nafasi ya pili
ilichukuliwa na Hussein Madroback ambaye alizawadidiwa pesa taslimu shilingi
laki moja(100,000).Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Merczedec Amadeus bada ya
kumfunga Abdul Faraji kutoka Dodoma 4 – 2, na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu
Shilingi elfu hamsini na Abdu Faraji kujitwalia nafasi ya nne ambapo
alizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi elfu ishirini na tano (25,000).
Klabu shiriki katika
mashindano hayo zilikuwa ni pamoja na Klabu ya Fuoni kutoka Zanzibar, Mpo
Afrika kutoka Temeke, Kayumba kutoka Ilala, Sunset kutoka Temeke, Topland
kutoka Kinondoni, BMK kutoka Temeke, Y2K kutoka Ilala, Mboya kutoka
Kilimanjaro, Jaba kutoka Kinondoni, Soccer City kutoka Kinondoni, Tabata kutoka
Ilala, Kurasini City kutoka Temeke, Mbezi Beach Inn kutoka Kinondoni, MKWAJUNI
KUTOKA Kinondonmi na Dodoma kutoka
Dodoma.
Akizungumza na wachezaji
pamoja na mashabiki wakati wa kukabidhi zawadi, Mgeni rasmi na Mwenyekiti wa
Chama cha Pool Tanzania, Isaach Togocho aliwapongeza waandaaji wa mashindano ya
Pool nanenane ambayo yalijulikana kama “88” Pool Competitions 2016 kwa
kufanikisha mashindano hayo kwa ubora wa juu na hamasa kubwa na kuwaomba wadau
wengine kuiga mfano huo ambao utafanya mchezo kusonga mbele.
Aidha Togocho aliwaomba
wachezaji na washika dau kuhakikisha wanakemea wale wote wanaosababisha
kuonekana mchezo wa pool kuonekana wa kihuni hususana wacheza Kamari ambao
hawafuati hata sharia ya nchi ya muda maalumu wa kucheza mchezo huo hata
ikibidi kuwapeleka kwenye vyombo vya sharia.
Post a Comment