Meneja wa
Bia ya Kilimanjaro Primium Lager, Pamela Kikuli akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa uzinduzi wa Kampeni maalumu ya “Friji ya Ushindi”ambayo
Watanzania tukishinda inafunguliwa na kugawiwa bia za Kilimanjaro Primium Lager
bure, iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki katika Bar ya Juliana Mbezi Beach jijini
Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya
Bia Nchini kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Primium Lager imezindu Kampeni ya Friji ya Ushindi kwa
wadau wote wa soka ili kuhamasisha Watanzania kuishangilia Tanzania ishinde iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika
Bar ya Juliana Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Primium Lager, Pamela
Kikuli alisema hii ni Kampeni maalumu kwa wadau wote wa soka ili kuweka
uzalendo mbele kama Watanzania kuishangilia timu yao na Tanzania ikishinda
friji inafunguliwa na kugawiwa bia za Kilimanjaro Primium Lager bure kabisa.
Alisema
Kikuli Tbl kuitia Bia yake ya Kilimanjaro wanaamini Watanzania wakiweka
uzalendo mbele ni lazima tutashinda hivyo ni wakati maalumu kwetu watanzania tushikamane
na lazima tutafika mbali.Kampeni hii tumeweka friji ya ushindi sehemu
mbalimbali ambazo tutataja hapo baadae zikiwa zimejaa bia na Watanzania
tukishinda friji ya ushindi inafunguliwa na kugawa bia za Kilimanjaro bure.
Kikuli alisema
TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro wakao tayari kutoa hamasa kwa Watanzania
wadau wa soka kuungana nao kila Tanzania inavyofanya vizuri kwenye soka.
|
Post a Comment