BALOZI WA CASTLE LAGER AFRICA 5s TANZANIA, IVO MAPUNDA AHAMASISHA WENYE BAA KUUNDA TIMU BORA ZITAKAZOWAKILISHA BAA ZAO KWENYE FAINALI YA BONANZA KUBWA LA CASTLE LAGER AFRICA 5s 2019.
Balozi wa Castle Lager Africa 5s, Ivo Mapunda |
BALOZI wa Castle Lager Africa 5s nchini Tanzania, Ivo Mapunda amewaomba wamiliki wa Baa kuunda timu bora za kiushindani zitakazowakilisha Baa zao kwenye fainali ya Bonanza kubwa litakayoshirikisha timu 32 kutoka Baa tofauti za jijini Dar es Salaam na kupata timu moja itakayowakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania mwaka huu wa 2019.
Mapunda aliyasema hayo jana kwa Waandishi wa
habari wakati akijiandaa rasmi na ziara ya kutembelea Baa 60 za jijini Dar es
Salaam zilizoingia kwenye mchakato wa kiushindani kupitia promosheni zinazoendelea
kwenye Baa hizo na kuwaomba wamiliki hao wajitahidi sana kuunda timu bora kwani
tunatarajia kuwa na ushindani mkubwa ambao mwisho wa siku utatupatia timu moja
kutoka Baa moja itakayotuwakilisha Watanzani kwenye mashindano ya Africa.
Mashindano haya yanafanyika
hapa nchini kwa mara ya kwanza lakini ikiwa ni mara ya pili kwa Tanzania
kushiriki chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia nhini(TBL) kupitia bia yake ya
Castle Lager. Hata hivyo yamekuwa yakifanyika katika nchi nyingine za Afrika hivyo
kwa fursa tuliyopewa Watanzania ya fainali za Africa kufanyika Tanzania
nawasihi wamiliki wa Baa shiriki tutambue Bingwa wa fainali ya Bonanza
atatuwakilisha Watanzania wote na kwa maana hiyo uundaji wa timu zetu na
maandalizi kwa ujumla yanapaswa kuwa mazuri, ‘alisema Balozi wa Castle Lager
Tanzania,Mapunda’.
“Mwaka jana tulishiriki
mashindano haya kwa mara ya kwanza na kupata mwakilishi aliyeshiriki katika
michuano ya Kimataifa ya Afrika, yaliyofanyika nchini Zambia kwa kuzikutanisha
timu za Afrika Kusini, Zimbabwe, Swaziland Lesotho na wenyeji Zambia”.
Binafsi
niwapongeza sana Wadhamini wa mashindano haya Castle Lager kwa kudhamini
mashindano haya ambayo yanawapa fursa wanywaji wao kushiriki michezo ambayo
mwisho wa siku unatupa nafasi ya kuitangaza nchi yetu ya Tanzania lakini pia
niwashukuru sana kwa kuniona mimi kama nastahili kuwa Balozi wa Castle Lager
Africa 5s nchini Tanzania.
“Nafahamu Mchakato wa kupata timu
zitakazoshiriki katika bonanza hilo umeboreshwa zaidi mwaka huu, ambapo
washiriki watapatikana kupitia katika promosheni zinazoendelea katika baa
mbalimbali jijini Dar es Salaam”.
Ili kuingia 32
bora, moja ya kigezo muhimu ni kufanya mauzo mengi ambapo kutakuwa na makasha
maalumu katika baa husika kwa ajili ya kukusanyia vizibo baada ya mteja kununua
bia ya Castle Lager.
Niwaombe
watanzania kutumia nafasi hii, ambayo itawapa wakati mzuri wa kutimiza ndoto
zao. Wakati mwingine fursa kama hizi ni nadra sana.
Post a Comment