NICHORAUS NGOROMA MABINGWA MBIO ZA BALIMI MITUMBWI UKEREWE.
![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mery Tesha... |
Na Mwandishi wetu,Kagera.
KIKUNDI cha Wanaume
wapiga kasia cha Nichoraus Ngoroma Kisiwa cha Ukerewe kimeibuka na
ubingwa katika fainali za mashindano yambio za mitumbwi chini ya udhamini wa
bia ya Balimi Extra Lager zijulikazo
kama “Balimi Boat Race 2014” na hivyo kikundi hicho kuzawadiwa pesa taslimu
Shilingi 900,000/= pamoja na kuwakilisha Kisiwa hicho kwenye fainali za Kanda
zinazotarajiwa kufanyika Desemba 6 mwaka huu jijini Mwanza.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha Kapina Kagari
ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/= pamoja na kuwakilisha
Kisiwa cha Ukerewe katika fainali za Kanda jijini Mwanza pia, wakati nafasi ya
tatu ilichukuliwa na kikundi cha Athumani Malemo ambacho kilizawadiwa pesa
taslimu Shilingi 500,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha
Mashauri Saidi ambacho kilizawadiwa Shilingi 400,000/=
Nafasi ya tano hadi ya tisa walipewa kifuta jasho cha pesa
taslimu Shilingi 250,000/= kila kikundi ambavyo ni Asante Robert, Ladsilaus
Musimu, Benedicto Aniseti, Gervas Kulwa, Simon Fundi na Silvari Sasieli.
Upande wa Wanawake kikundi cha Muhate Mwocha kilifanikiwa
kutwaa ubingwa na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 700,000/= pamoja na
nafasi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda jijini Mwanza.Nafasi ya pili
Wanawake ilichukuliwa na kikundi cha Mlanzi Mussa ambao walizawadiwa Shilingi
600,000/=,washindi wa tatu ni kikundi cha Joyce Makalu ambao walizawadiwa
Shilingi 400,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Beatrice
Kalomba ambao walizawadiwa Shilingi
300,000/= na nafasi ya tano hadi ya kumi walizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi
200,000/= kila kikundi ambavyo ni kikundi cha Pili Masitu, Adventina Elias,
Jesca Jose, Veronica Machumu,Juliana Petro na Maria Mabagara.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi Mkuu wa Wilaya ya
Ukerewe, Mery Tesha kwanza alitoa
shukrani kwa Kampuni ya bia nchini(TBL) kupitia bia ya Balimi Extra Lager ambao
ndio wadhamini wa mashindano hayo na kuwaomba waendelee kudhamini kwani
yanaleta hamasa umoja na udugu kati yetu kuiachilia mbali afya na kipato
kinachopatikana kama zawadi mara baada ya mashindano.
Tesha alisema washindi waliopatikana wakaiwakilishe vyema
Ukerewe na wahakikishe wanarudi na ushindi na wale ambao hawakupata nafasi ya
kushinda wajiandae kwa mashindano mengine mwakani.
Tesha alimaliza kwa kuwaomba zawadi walizopewa wakazitumie
kwab maendeleo yao kwani huo ni mtaji tocha kwa mtu anayeweza kujishughulisha.
Fainali za Kanda za mbio za mitumbwi zijulikanazo kama
“Balimi Boat Race 2014” zinatarajiwa kufanyika
Desemba 6, mwaka huu jijini Mwanza katika ufukwe wa Mwaloni.
![]() |
| Washindi wa kwanza wa mbio za makasia wa Kisiwa cha ukerewe kikundi cha Nichoraus Ngoroma wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi mwishoni mwa wiki. |


Post a Comment