Kikosi cha wachezaji wa Airtel Rising Star Tanzania chawasili nchini kikitokea jijini Lagos Nigeria
Mabigwa wa michuano ya Airtel Rising Stars Afrika kwa upande wa wasichana Timu ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jana usiku. |
Kikosi cha timu ya Airtel Rising Stars cha Tanzania wakiwa kwenye Bus tayari kwenda hotelini mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Julius Kambarage nyerere jana usiku. |
Mzazi wa mchezaji wa kike, Donisia Daniel akimpokea mwanae kwa furaha. |
Athuman Hamis Balozi wa Usalama Barabarani
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Simu ya Airtel imesema kuwa itahakikisha suala la Usalama barabarani linazingatiwa na jamii ya Watanzania ili kupunguza ajali za barabarani .
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel,Beatrice Mallya kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya UsalamaBarabarani,yanayofanyika Jijini Mwanza.
Alisema kama wadau wa usalama barabarani,wamedhamini maadhimisho hayoili kuwezesha jamii kupata elimu na uelewa kuhusu matumizi yabarabara,sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani katika kupunguza ajali nchini.
alisema ajali nyingi nchini zinachelewesha maendeleo na kupunguza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
“Sisi kama wadau tumedhamini maadhimisho haya kwa mwaka wa tano mfululizo,lengo letu tunataka jamii ipate uelewa na hatimaye kupunguza ajali za barabarani zinaoweza kuepukika,ndiyo sababu tuko hapa,”alisema.
Alisema kutokana na kuonesha umahiri wameanzisha mfumo mpya wa ulipiaji wa leseni za magari kwa kupitia njia ya Airtel Money.
Twiga Stars kuanza na Wazambia Afrika
TIMU ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) imepangiwa kucheza na Zambia katika mechi za kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika mwakani nchini Namibia.
Twiga Stars itaanzia ugenini jijini Lusaka ambapo mechi ya kwanza itachezwa kati ya Februari 13 na 15 mwakani wakati ile ya marudiano itafanyika kati ya Februari 28 na Machi 2 mwakani jijini Dar es Salaam.
Iwapo Twiga Stars itafanikiwa kuitoa Zambia, raundi ya pili ambayo ndiyo ya mwisho itacheza na mshindi kati ya Botswana na Zimbabwe. Mechi ya kwanza itakuwa Dar es Salaam kati ya Mei 23 na 25 mwakani wakati ile ya marudiano itakuwa kati ya Juni 6 na 8 mwakani.
Nchi 25 zimeingia katika mashindano huku mabingwa watetezi Equatorial Guinea, makamu bingwa Afrika Kusini na Cameroon iliyoshika nafasi ya tatu katika fainali zilizopita zikiingia moja kwa moja katika raundi ya pili.
Mh. Balozi Batilda S. Burian akiwa katika zoezi la kutolewa damu pamoja na watanzania wengine aliyoambatana nao.
Balozi
wa Tanzania nchini Kenya Mhe Batilda S. Burian, leo ameongoza umati wa
Watanzania waishio hapa Nairobi, Kenya, kujitolea damu kwa ajili ya
kuwasaidia waathirika wa tukio la ugaidi lililotokea Tarehe 21 Septemba
2013 jijini Nairobi Kenya, ambapo hadi sasa zaidi ya watu 62
wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 179 wamejeruhiwa vibaya na wengi
wao bado wanaendelea kupata matibabu katika hospitali za Aga Khan
University Hospital, Hospitali ya Nairobi ( Nairobi Hospital), na
Hospitali ya MP Shah.Picha Kwa hisani ya Michuzi Blog
Katika
tukio hilo pia Mtanzania, Bwana Vedastus Nsanzungwanko, Meneja, Child
Protection, UNICEF ni mmoja wa wale walioathirika na tukio hilo ambapo
alijeruhiwa kwa risasi na magruneti katika miguu yake yote miwili. Hivi
sasa Bwana Vedastus amelazwa katika hospitali ya Aga Khan, Nairobi na
anendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Post a Comment