MO AVUNJA BENKI
WANANUKA fedha! Ndiyo utakavyoweza kusema kwa wachezaji wa Simba baada ya kupewa shilingi milioni 300 na mwekezaji wao bilionea, Mohammed Dewji ‘Mo’ kufuatia kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Hiyo, ikiwa ni siku moja tangu timu hiyo ifuzu katika hiyo michuano mikubwa Afrika kwa kuwafunga wapinzani wao AS Vita mabao 2-1 mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, mabao ya Simba yalifungwa na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Mzambia, Clatous Chama huku lile la Vita likipachikwa na Kasadi Kasengu.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo limezipata Championi Jumatatu, wachezaji hao watapewa mamilioni hayo baada ya ushindi wa michezo mitatu ya hatua ya Robo Fainali katika Kundi D lenye timu nne.
Mtoa taarifa huyo alisema wachezaji hao waliahidiwa kupewa Sh milioni 100 kwa kila mchezo watakaoshinda na kutokana na kushinda michezo mitatu, basi watachukua Sh milioni 300.
Aliongeza kuwa, wachezaji hao awali waliahidi w a kupewa Sh milioni 100 wa kishinda na sare milioni 50 ambazo hizo wamezikosa kutokana na kufungwa michezo mitatu ya ugenini na AS Vita, Al Ahly zote walifungwa mabao 5-0 kabla ya kufungwa tena mabao 2-0 na JS Saoura.
“Kabla ya kuanza kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, viongozi wakiongozwa na mwekezaji wetu, waliwapa ahadi ya fedha wachezaji wetu kama motisha ili wapambane ndani ya uwanja.
“Ahadi hiyo waliyopewa ni shilingi milioni 100 kwa kila mchezo watakaoshinda na shilingi milioni 50 timu ikitoa sare ikiwemo nyumbani na ugenini na lengo ni kuona timu inapata matokeo mazuri.
“Hivyo, baada ya kufanikiwa kufuzu hatua hiyo ya makundi, tukipata pointi 9 baada ya ushindi wa mchezo wetu uliopita, watakuwa wamekamilisha mechi tatu walizoshinda na kufikisha shilingi milioni 300 ambazo watapewa wachezaji wetu,” alisema mtoa taarifa huyo.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Mbelgiji, Patrick Aussems alisema: “Nafurahia kuona wachezaji wangu wakipambana na kufanikiwa kutengeneza rekodi ya timu na nchi kwa ujumla.
“Na hiyo imetokana na umoja, ushirikiano kati ya wachezaji, Benchi la Ufundi na viongozi ambao wamekuwa wakitoa motisha ya fedha katika kuwahamasisha ili wapambane.”
Post a Comment