Kivule Veteran, Tanganyika Internatioanal School kuoneshana ubabe Ijumaa
Nahodha ambaye pia ni golikipa namba moja wa
timu ya Kivule Veteran, Ali Kipande (kulia), akijandaa kudaka mpira katika mechi
kirafiki dhidi ya Kitunda Veteran, iliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi
Kitunda, Dar es Salaam.
Timu ya Kivule Veteran ikiwa mazoezini leo kwenye
Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Misitu, Dar es Salaam, kujiandaa na mechi ya
kirafiki dhidi ya Shule ya Kimataifa ya Tanganyika Veteran inayotarajiwa
kufanyika Ijumaa, Uwanja wa Shule ya Tvanganyika, Masaki, Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu TIMU ya Kivule Veterani iko kwenye mazoezi makali kujiandaa kwa mechi kabambe na timu ya maveterani ya Shule ya Kimataifa ya Tanganyika ya Masaki Dar es Salaam. Mechi hiyo ya kirafiki ambayo kwa wiki mbili imezua gumzo jijini, inatarajiwa kufanyika Ijumaa ijayo Novemba 2, kwenye Uwanja wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika, Masaki. Akielezea wakati wa mazoezi yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Misitu, Nahodha wa timu ya Kivule Veterani, Ali Kipande, alisema timu yake imejiandaa vya kutosha kupambana na Tanganyika Veteran ambayo itaundwa kwa asilimia kubwa na Walimu pamoja na Wafanyakazi wa shule hiyo. "Timu yatu imekuwa ikijifua vilivyo kwa takribani wiki mbili sasa kujiweka imara kupambana na timu hiyo. Tunawaahidi wakazi wa Kivule kuwa hatutawaangusha tutawafunga Tanganyika mabao kibao,"alijinasibu nahodha huyo huku kauli yake hiyo ikiungwa mkono na wenzie kwa kumpigia makofi. Alisema Tanganyika Veterani waliwaletea mwaliko wa kucheza nao takribani wiki mbili zilizopita, baada ya kupata sifa za timu ya Kivule Veterani ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika mechi mbalimbali ilizocheza. Kipande ambaye pia ni golikipa namba moja wa Kivule Veterani, alisema kuwa Uongozi wa Tanganyika Veterani umeahidi kupeleka mabasi mawili kubeba wachezaji na mashabiki wa timu ya Kivule ambayo ipo Jimbo la Ukonga, Ilala, Dar es Salaam. Aliwataja baadhi ya wachezaji wa kutumainiwa wa timu hiyo kuwa ni.Mtangazaji wa TBC, Jesse John, Abdalah MkambakuNyakasagani Masenza, Quresh Ufunguo, Peter Mwenda, Richard Mwaikenda, Hassan na Sanga. Kwa mujibu wa Kipande alisema kuwa mechi hiyo ya kukata na shoka itaanza saa 10 jioni, hivyo aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika makao makuu yao yaliyopo Kwa Mnyamwezi karibu na Saluni ya Mchezaji maarufu wa Simba, Quresh Ufunguo ambaye pia ni kocha mchezaji wa timu hiyo. Aliwataka wafike hapo majira ya saa 7 mchana, na waliopo mjini wajitahidi waungane nao kwenda Masaki wakitokea huko huko makazini. |
Post a Comment