ad

ad
SIKIA HII

Akina mama kwa kujisahau wamezidi

Jamani kama kuna watu wanaoongoza kwa kujisahau, basi zaidi ni wanawake .Hilo halina ubishi kwasababu wengi wetu tumeshuhudia jinsi wanavyokuwa na vipochi vidogo vya hela au wakati mwingine wanafunga pesa hizo kwenye kitambaa.

Na wakati mwingine kwenye mafundo ya khanga, lakini cha ajabu anaweza akasahau kabisa kifushi chake cha pesa alipokiweka anapohitaji na ukachangaa akipekua hata kuivuruga nyumba mara anapokihitaji.

Kujisahau kwao si katika pesa, hata katika vifaa vya jikoni, wanawake wanaweza kusahau alipokiweka kisu na kuanza kukisaka asikione mpaka kufikia hatua ya kwenda kuazima kwa jirani.

Hiyo ni mifano michache ambayo nimeamua kuitoa ili kuwaeleza jinsi MN alivyopata shida hivi karibuni kutokana na tabia hiyo ya kusahau kwa wanawake.

Kama ilivyo ada ya MN kupita huku na kule, alikumbana na adha hiyo ya kusahau kupita kiasi kwa wanawake na ndio sababu leo MN ameamua kuweka hadharani hili ili wanawake wenye tabia hiyo wapunguze na kuwa makini kidogo.

Hiyo ni kutokana na mkasa huu, MN kama kawaida yake ya kupita huku na kule kusaka ugali wake, basi alikuwa katika daladala moja lifanyalo safari zake Sinza Gongolamboto.

Kama inavyohahamika namna daladala hizi hasa nyakati za jioni huwa zinajaza sana na wakati mwingine ni aghalabu kwa mtu unayepandia vituo vya katikati kupata nafasi ya kukaa.

Sasa kituko ambacho kimemfanya MN leo alonge, ni pale alipotaka kuachiwa motto mdogo wa kama miaka miwili hivi baada ya uungwana wake wa kumpokea mama mwenye mtoto huyo.

MN alikuwa amepata kiti kwasababu yeye alitoka mwanzo wa safari za daladala hilo pale Afrika Sana, kama ujuavyo daladala hizi na kujaa kwake na wakati mwingine wanawake wenye watoto hupenda kupanda hivyo hivyo wakidhani watapishwa.

Basi hilo halikuwa kwa mama huyu, yeye alipanda gari moja na MN maeneo ya ‘Kwa Mtogole’ huku tayari ikiwa imejaa nay eye akiwa na motto wake huyo mdogo wa kiume.

Kama ilivyo kawaida ya kondakta, yeye hakumjali mama ana mtoto wala nini alikuwa akimtaka kusogea huku akichombeza huo ndio usafiri na hiyo ni daladala ya mwisho zingine haziji zinaogopa foleni.

Nadhani wapo waliomuonea huruma, lakini wakifiria kumpisha waliona ni mateso na adha ya kusimama nap engine walikuwa wakienda mbali.

Lakini pengine walikuwapo waliojisemea moyoni kwanini apande gari iliyojaza, hilo sijui lakini kwa jinsi kil mmoja alivyouchuna kumpisha, majibu yote hayo yanawezekana.

Baada ya kuona hali hiyo huku MN naye akiwa ni miongoni mwa watu ambao hawakutaka kumpisha, aliona msaada pekee anaoweza kumpatia ni kusaidia yule mtoto.

Ehee kweli MN ndipo alipoamini kwamba wanawake wengi wanajisahau mno kwani baada ya safari kiasi na kufikia kituo cha Kigogo, yule mama alishuka na kuanza kuondoka yaani akijisahau kabisa kama alikuwa na mtoto.

Wakati hilo likitokea, MN naye hakuwa na wazo lolote kwasababu alikuwa akiendelea na safari hadi mwisho hivyo aliamini mama wa mtoto kama atashuka njiani atamhitaji mwanawe na kama anakwenda mpaka mwisho watakuwa pamoja.

Ehe, ghafla inasikika sauti ya mtoto, mama, mama MN na abiria wengine wanamshangaa lakini wanashtushwa na mama yule ndio anakumbuka huku gari ikikaribia kuondoka na kufanya MN amtoe mtoto dirishani akipokelewa na kondakta na kumpatia yule mama.

Jamani akina mama kuweni makini, hii ni hatari kama imefikia hata kumsahau mwanao.
xxxxxxxMWISHO

No comments