ad

ad
Juma Nature kuipagawisha Kitonga Krismas

Na Mwandishi Wetu

KITONGA kumekucha! Mwanamuziki mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Juma Nature Krismasi hii anatarajiwa kufanya onyesho la muziki kwenye Ukumbi Starcom Kitonga Comfort mkoani Iringa.

Akizungumza na Mtanzania jijini Dar es Salaam jana, Meneja Masoko wa Hoteli ya Kitonga Comfort, Yusuf Waziri maarufu kama Ngedere alisema maandalizi ya onyesho hilo yameshakamilika.

“Kiingilio katika onyesho hilo ni shilingi 5,000 na usalama wa mashabiki na mali zao umewekwa sawa hivyo wasiwe na shaka,” alisema Ngedere.

Ngedere aliongeza kuwa onyesho hilo la muziki kutoka kwa Juma Nature litaanza saa mbili usiku hadi lyamba.

Mbali na onyesho hilo, mchana kutakuwa na shoo ya watoto wadogo ambapo watashindana katika uchezaji wa kiduku na mshindi atapata zawadi ya baiskeli, wa pili Sh 20,000 na mshindi wa tatu Sh 10,000. Kingilio kwa watoto ni Sh 1,000 na mtu mzima Sh 2,500.
XxxxxxxxMWISHO

Yanga kuanza mazoezi leo

Na Kambi Mbwana

KLABU ya Yanga inatarajia kuanza mazoezi leo kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom chini ya Kocha wake Mkuu Kostadian Papic baaada ya kumaliza mazoezi ya viungo (GYM) waliyoanza wiki iliyopita.

Akizungumza na Mtanzania, ofisa habari wa klabu hiyo , Louis Sendeu, alisema mikakati yao ni kuhakikisha wanaingia kwenye ngwe ya pili wakiwa na kikosi chenye nguvu ya kushinda kila mechi na kuibuka na ubingwa wa ligi hiyo.

“Tuliaamua kuwafanyisha mazoezi ya viungo wachezaji wetu tukiamini yatawajenga vema kimisuli na kuwa na uwezo wa hali ya juu wakati wa mzunguko huu wa lala salama” alisema Sendeu.

Alisema baada ya mazoezi hayo, Papic ndiye atakuwa mwenye jukumu la kupanga namna ya program anazohitaji baada ya wachezaji kuanza mazoezi huku akisubiri kuwachanganya na wale waliopo Kilimanjaro Stars iliyokuwa ikishiriki michuano ya Challenge iliyomalizika jana.
XXXXXXMWISHO



Mkwasa alonga kuhusu CECAFA

Na Jennifer Ullembo

KOCHA Mkuu wa timu ya wanawake Twiga Stars ,Charles Boniface Mkwasa ameisifu michuano ya Challenge na kusema imeleta mwamko katika soka nchini.


Akizungumza na Mtanzania,
Mkwasa alisema michuano hiyo imeletea changamoto hasa kwa timu zetu kwani tumeona jinsi wachezaji walivyojitahidi kuhakikisha wanafika fainali..

Mkwasa alisema timu zetu zimejifunza kutoka kwa timu nyingine zilizoshiriki michuano hii mwaka huu .

“Tumejifunza mengi kupitia michuano hii timu zetu kutoka Zanzibar na Tanzania Bara zimeonyesha juhudi ingawa moja wapo imeshindwa kufika kileleni”alisema Mkwasa

Mkwasa ameisifu Kili Stars kwa hatua iliyofikia kwa kupata nafasi ya kushiriki na kuingia fainali za michuano hiyo , aidha kocha huyo aliwaomba mashabiki kuwa na mori ya kushangilia timu zao pindi ziwapo uwanjani ilikuwapa moyo wachezaji wao

Akizungumzia timu ya Twiga Stars, alisema bado wachezaji wapo mapumzikoni.

“Timu yetu bado haijapanga ratiba yoyote tunasubiri kuweka sawa mambo yetu na TFF kwanza”alisema Mkwasa
XXXXMWISHO

‘Chokoraa, Kalala Junior watovu wa nidhamu’


Na Kambi Mbwana

MKURUGENZI wa Twanga Pepeta, Asha Baraka amewajia juu wanamuziki wake wawili, Kalala Junior na Khalid Chokoraa akidai ni watovu wa nidhamu.

Akizungumza kwa hisia kubwa, mwanamama huyo amesema kwamba bendi yake haiwezi kuvumilia tabia hiyo kwa madai inaweza kuisambaratisha katika kona ya muziki wa dansi nchini, yenye ushindani wa hali ya juu.

Alisema tangu kuasisiwa kwa muungano huo, Kalala na Chokoraa wamekuwa na tabia ya kuondoka kazini kinyume cha utaratibu na sheria za kazi, hivyo adhabu hiyo ni siraha ya kuhakikisha wanakuwa na tabia njema.

“Usione Twanga imefikia hatua hii, ni muungano na ushirikiano kutoka kwa wadau wakiwamo wanamuziki wangu, hivyo ipo haja ya kuimaisha mshikamano wetu.

“Wanatakiwa wawe tayari kufanya kazi na upande mmoja, kuliko ndani ya wiki moja huonekani kazini kwako siku tatu, ukizingatia kwamba shoo kwa wiki hazizidi tano au nne,” alisema.

Katika muungano huo wa Mapacha Watatu, pia yupo mwanamuziki wa FM Academia, Wazee wa Ngwasuma, Jose Mara, Rais wa Kimara.

Xxx


Mbishi atambia single yake ya amebaka


Na Kambi Mbwana
MWIMBAJI wa Bongo Fleva nchini, Fredy Kaguo ‘Mbishi’ amesema kwamba kuanza kushika kasi kwa wimbo wake mpya wa ‘Amebaka,’ kuna mpa matumaini ya kuendelea kukaa juu.

Mbishi katika wimbo huo ameimba kwa pamoja na mkali wa Wanaume Family Juma Said Chege na Mohamed Mchopanga ‘Jay Mo’, mkali wa Wateule.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, mwimbaji huyo wa ‘Pombe’ na ‘Tozi wa Mbagala’ alisema kwamba hiyo ni mikakati ya kumfanya azidi kuwa matawi ya juu.

Alisema wimbo huo umekaa katika kiwango cha juu, huku akiimba na wakali katika fani hiyo ya muziki wa Bongo Fleva, inayozidi kupata umaarufu.

“Wasanii ni wengi na wote wanafanya juhudi kuendelea kufaanikiwa huku wadogo zetu nao wakitamani kuwa kama wenzao wenye majina.

“Naamini wimbo wangu umedhihirisha umakini wangu, huku nikiamini kwamba mambo yatazidi kuwa mazuri na kusimama kileleni kama nilipokuwa sasa,” alisema.

Mbishi ni kati ya makundi ya vijana wanaoishi kwa kupitia sanaa ya muziki wa Bongo Fleva na kuleta chachu kwa uwingi wa wasanii hao.

Mwisho

No comments