ad

ad
Martha Mlata akamilisha ‘Single ya JK

Na Muhidin Sufiani

MBUNGE wa Viti Maalum wa mkoa wa Singida, ambaye pia ni msanii wa nyimbo za Injili, Martha Mlata, amekamilisha single kwa ajili ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa ushindi alioupata kwenye Uchaguzi Mkuu uliomalizika Oktoba 30.

Single hiyo itajulikana kama hongera JK au Big Up JK, umerekodiwa katika Studio za Omega Production 2010 zilizopo Kinondoni Moroco kwa usimamizi wa muandaaji (Prodyuza) Amri Hing.

Akizungumza na Mtanzania, Mlata alisema katika wimbo huo amemshirikisha pia mpiga gitaa mahiri, Alex Sinkamba, ambaye ndiye aliyepiga magitaa yote ya single hiyo.

Alisema ameamua kutunga wimbo huo wa kumpongeza Rais baada ya kazi kubwa aliyoifanya ya kutangaza Ilani ya Chama cha Mapinduzi na kunadi Sera za chama hicho nchi nzima na hatimaye kuibuka na ushindi.

“Single hii maalum natarajia kumkabidhi rais kama zawadi yangu kumpongeza kwa ushindi hasa nikiamini ushindi wake ulikuwa ni wa haki kutoka kwa Mungu, kutokana na uongozi bora wa awamu ya kwanza ya uongozi wake, na kile kilichopangwa na mungu mwanadamu hawezi kukipangua hivyo kwa ushindi huu wa kutuongoza tena wananchi wa Tanzania, ndiyo maana nimefarijika na kuamua kumtungia wimbo wa kumpongeza.
XxxxxxxxxMWISHO

Ndumbaro: Nitaendelea kupeleka wachezaji nje

Na Mohamed Mharizo

WAKALA anayetambuliwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Damas Ndumabaro amesema ataendelea kupeleka wachezaji katika klabu ya Gefle FC ya Sweden.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ndumaro alisema hajajiaribia kufanya kazi na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.

“Kwa upande wangu sijajiharibia kufanya kazi na Gefle FC, aliyejiharibia ni Boban, mimi nitaendelea kufanya nao kazi kama kawaida,” alisema.

Alisema bado ana mpango wa kupeleka wachezaji wengi zaidi katika klabu hiyo lakini kwa sasa hali si nzuri ya kufanya usajili kutokana na kuwepo baridi kali.

“Boban amefanya mambo si ya kiustaarabu, na kiungwana amejiharibia mwenyewe, kwangu mambo yanaendelea,” alisema.

Boban alirejea nchini Julai mwaka huu na kusitisha mkataba wake na klabu hiyo. Inaelezwa mchezaji huyo kwa sasa ametimkia barani Ulaya kujaribu bahati yake huko baada ya kukosa kusajiliwa hapa nchini kupitia usajili wa dirisha dogo uliomalizika Novemba 30.
XxxxxxxxxMWISHO.


Mwape arudi kwao Zambia

Na Deborah Kajolo

MSHAMBULIA mpya wa klabu ya Yanga, Davies Mwape Musonda jana ametimkia kwao Zambia na atarudi Ijumaa kuungana na wenzake katika mazoezi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, unatarajiwa kuanza Januari 15 mwakani.

Ofisa habari wa Yanga, Louis Sendeu alizungumza na Mtanzania na kuthibitisha kuondoka kwa mchezaji huyo ambapo alidai kuwa ameomba ruhusa ili kuiaga rasmi familia yake kabla ya kuanza mazoezi ya moja kwa moja kujiandaa na ngwe hiyo ya mwisho.

Alisema alipokuja mara ya kwanza hakuwa amejiandaa moja kwa moja kwani katika mazungumzo kuna kuafikiana na kukataa.

“Magazeti yasije yakaanza kusema kuwa Mwape ametimka maana nyie hamkawii, ameenda kuona familia yake na kuchukua vitu vyake ili arudi rasmi kucheza soka sasa,” alisisitiza Sendeu.

Katika hatua nyingine, Sendeu alisema timu yao itaendelea na mazoezi yake leo katika Uwanja wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), kujiimarisha na ngwe hiyo ya pili.

Alisema wachezaji wote isipokuwa wale wanaoshiriki michuano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) wataendelea na mazoezi chini ya kocha wao mkuu, Kostadin Papic.

Yanga inayonolewa na Mserbia, Papic inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu nchini ikiwa na pointi 25 huku mabingwa watetezi, Simba wakiwa kileleni na jumla ya pointi 27.
XXXXMWISHO

Simba kuanza mazoezi leo

Na Kambi Mbwana

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara,timu ya Simba, leo itaanza mazoezi ya Gym, iliyopo Chang’ombe jijini Dar es Salaam chini ya kocha msaidizi Amri Said ‘Stam’.

Akizungumza jijini jana, ofisa habari wa klabu hiyo, Crifford Ndimbo, alisema mazoezi hayo ni maamdalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom itakayoanza Januari 15 pamoja na ile ya Mabingwa Afrika.

“Kesho (leo) timu itaanza mazoezi rasmi chini ya kocha msaidizi Amri hivyo wachezaji wote ambao hawako kwenye Challenge watakuwepo,”

“Naamini kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa na kuiweka timu vizuri, kabla ya kocha wetu Patrick Phiri, hajarejea kutoka kwao Zambia alikokwenda kwa likizo fupi,” alisema.
XxxMWISHO

TFF yakumbushwa ratiba daraja la kwanza

Na Jennifer Ullembo

SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF), limetakiwa kutoa ratiba ya timu zitakazoingia tisa bora katika mzunguko wa pili wa ligi daraja kwanza .

Akizungumza na Mtanzania, Katibu Mkuu wa Chama cha soka Iringa (IRFA), Eliud Mvela alisema TFF inatakiwa kutoa ratiba mapema kuepusha malumbano ya viongozi wa timu zinazoshiriki ligi hiyo.

Alisema hivi karibuni uongozi wa Timu ya Moro United umesikika ukijitapa kuwa timu yao ni moja wapo ya timu zitakazo ingia tisa bora katika mzunguko wa pili.

Katibu huyo alisema uongozi wa timu hiyo unatangaza uongo kwani katika msimamo wa ligi uliomalizika timu hizo zimezidiana pointi kidogo sana .

Mvela alisema ili kuondoa utata huo, TFF inatakiwa kutangaza ratiba mapema kuepusha malumbano yasiyokuwa na msingi kwani Moro Unied haipaswi kujitangazia wakati bado ratiba haijatolewa .

Katibu huyo aliuponda uongozi wa Moro United kwa kujiongezea pointi na kusema timu hiyo ilimaliza mzunguko wa kwanza ikiwa na pointi 15 kwa kufungwa mabao tisa na kushinda mabao kumi na moja tu .

“Nashangaa Moro wanavyojitapa wakati sisi tunapointi sawa na wao ila tumepishana katika ufungaji na kufungwa”alisema Mvela
XxxxxxxMWISHO

African Lyon yajutaa

Na Jennifer Ullembo

UONGOZI wa Timu ya African Lyon umesikitika baada ya kushindwa kuwasajili wachezaji wawili kutoka nchini Kenya.

Akizungumza na Mtanzania jana Mkurugenzi wa timu hiyo Charles Otieno alisema walishindwa kuwasajili wachezaji hao baada ya kuchelewa kufatilia vibali vyao.

Wachezaji hao ni George Odhiambo anayechezea timu ya Gol Mahia na Ezekieli Odera kutoka KBC. Alisema jitihada za kuwasajili zilishindikana baada ya kuchelewa kufuatilia vibali vyao na muda wa usajili dirisha dogo ukiwa umepita.

Alisema baada ya kushindwa kuwasajili wachezaji hao, imefanikiwa kuwanasa Hamis Yussufu kutoka AFC, Shabani Aboma na Zahoro Pazi wa Mtibwa Sugar pamoja na John Njama kutoka TMK United.
xxxxxxMWISHO




1.

No comments