Habari zote na Mohamed Mharizo
Mkutano Mkuu Pan African Desemba 19
TIMU ya soka ya Pan African ya jijini Dar es Salaam, inatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa wanachama Desemba 19, mwaka huu.
Akizungumza jijini jana, Katibu Mkuu wa timu hiyo, Saad Mateo, alisema uamuzi wa kufanyika mkutano huo umefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji, kilichofanyika juzi.
Alisema mkutano huo ni wa kawaida na hufanyika kila mwaka ambapo agenda kuu ya mkutano ni kuhusu maendeleo ya timu na mapato na matumizi.
“Ili wanachama wahudhurie mkutano huo, wanapaswa pia kulipia kadi zao mapema, wasisubiri hadi kipindi cha uchaguzi ndio wafanye hivyo,” alisema.
Timu hiyo kwa sasa inafanya mazoezi katika Shule ya Sekondari Azania, kwa ajili ya Ligi ya TFF Mkoa wa Dar es Salaam, chini ya Kocha Mkuu, Likembe Njohole.
xxxxxxMWISHO
New Boys yachapwa 1-0
TIMU ya soka ya New Boys ya Ilala Bungoni, juzi ilikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Shein Rangers ya Sinza, katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Sinza Darajani.
Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu Faki Haji, inajiandaa na Michauno ya Vijana wilayani Ilala, inayosimamiwa na Chama cha Kuendeleza Soka wilayani humo (IDYOSA).
Akizungumza jana na Mtanzania, Mwenyekiti wa timu hiyo, Hamis Mwaita, alisema mchezo huo ni maandalizi kwa ajili ya ligi ya vijana na kuandaa timu yao.
“Lengo letu ni kupata michezo mingi ya kirafiki, na hii itasaidia wachezaji wetu kupata uzoefu katika ligi,” alisema.
Timu hiyo inaundwa na wachezaji chipukizi chini ya Mlezi Mkuu ambaye ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu.
XXXXXXMWISHO
Moro United kuingia kambini Desemba 15
TIMU ya soka ya Moro United, inatarajia kuingia kambini Desemba 15 kujiandaa na Fainali ya Ligi Daraja la Kwanza hatua ya Tisa Bora.
Timu hiyo, iliyowahi kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ilifuzu kucheza hatua ya tisa katika Ligi Daraja la Kwanza kwa kufikisha pointi 15.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hassan Banyai, alisema ni wakati wa wadau wa soka kuisaidia timu hiyo ili iweze kurejea Ligi Kuu.
“Tushirikiane kuisaidia timu yetu, hili ni jukumu letu wote na si la viongozi pekee, mafanikio yakija wote hufurahia, sasa tufanikishe mafanikio hayo,” alisema.
Timu hiyo ilianza mazoezi jana kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Tabata.
XXXXXXXXMWISHO
JM Mbeta kupiga kambi Panandi Ilala
BENDI ya muziki wa Dansi ya MJ Mbeta, inatarajia kupiga kambi kwenye Ukumbi wa Panandi, uliopo Ilala kwa ajili ya maonyesho yake.
Akizungumza na Mtanzania, mmiliki wa bendi hiyo, ambaye pia ni Mwanamuziki mkongwe, Julius Mzeru, alisema watakuwa wakipiga kwenye ukumbi huo kila Alhamisi.
“Tunahitaji kujitangaza na kuwa karibu na wadau wa muziki wa dansi nchini, hivyo tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi ili kushuhudia muziki wetu,” alisema.
Aliwataka mashabiki wa muziki wa dansi wawaunge mkono na watawapa burudani ya aina yake na wala hawatowaangusha.
Bendi hiyo pia inatarajia kuanza ziara za mikoani kwa ajili ya kuwatambulisha wanamuziki wa bendi hiyo.

Post a Comment