Majimaji kuweka kambi Msumbiji
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya soka ya Majimaji ya mkoani Ruvuma, Desemba 15 inatarajia kwenda nchini Msumbiji kuweka kambi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Tayari, timu mbalimbali za ligi hiyo nchini zimeanza mazoezi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi hiyo ambapo vigogo wa soka Simba na Yanga pia wameanza mazoezi ya viungo ‘gym’.
Makamu Mwenyekiti wa Majimaji, Ahmed Dizumba alizungumza na MTANZANIA na kusema wakiwa Msumbiji watacheza mechi tatu za majaribio na timu mbalimbali katika miji miwili nchini humo.
Dizumba alisema mechi hizo tatu watacheza na timu za miji ya Nampula na Lichinga ambazo wanaamini zitawasaidia katika kujua upungufu wao na kufanya marekebisho.
Alisema watakaa Msumbiji mpaka Januari 10, mwakani ambapo watakuwa wamebakiza siku tano kabla ya kuanza ligi hiyo iliyopangwa kurudi viwanjani, Januari 15.
“Tutaenda na makocha wetu, Sebastian Mkoma tuliyemuajiri hivi karibuni na kocha msaidizi Peter Mhina hiyo yote ni katika kuhakikisha kuwa tunafanya vizuri katika ligi hiyo,” alisema Dizumba.
Wakati huo huo, Dizumba alisema wanatarajia kumuajiri Mkenya Razak Siwa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, hivyo kama watafanikiwa katika hilo Mkoma atakuwa kocha msaidizi.
Alisema taratibu za kumpata kocha huyo zipo mbioni tayari ameshawatumia vyeti CV, ambazo wamezifanyia kazi na sasa wanasubiri Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), iwaruhusu kumtumia.
Majimaji wamesajili wachezaji watano katika usajili wa dirisha dogo ambao ni mshambuliaji wa Simba, Mohammed Kijuso, mchezaji huru Ulimboka Mwakingwe, Patrick Betwel, Kassim Kilungo aliyetoka Azam FC, Yahaya Shaban kutoka Segera Tanga.
xxxxxMWISHO
ZFA yaibua hoja ya Uanachama FIFA
Na Mohamed Mharizo
KATIBU Msaidizi wa Chama cha Soka Zanzibar, Masoud Attai Masoud ameibua upya hoja ya chama hicho kujiunga na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Akizungumza Dar es Salaam jana, Attai alisema kutokana na kiwango kizuri cha soka visiwani humo wana kila sababu ya kupewa uanachama huo na Fifa.
“Zanzibar ipo juu katika soka, tuna kila sababu ya kupata uanachama wa Fifa, kwani suala letu tulilipeleka tukiwa na Tenga, (Rais wa TFF).
“Hivyo ni wakati wa Wazanzibar wote kusubiri ‘positive answer’ wala suala hili haliwezi kuleta mgogoro, naamini tutafanikiwa”, alisema Attai.
Wakati huo huo, Attai aliweka wazi kutetea wadhifa wake wa Katibu Msaidizi wa ZFA katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Desemba 31 mwaka huu.
“Zanzibar tumetoka mbali, vijana wetu sasa wanacheza vizuri, tumekubalika Afrika Mashariki na hii ndio sababu ya mimi kuhitaji nafasi hii ili niendeleze soka zaidi.
“Tuna programu nzuri za kuendeleza soka la vijana naahidi kuwa na timu bora ya Zanzibar ambayo viwango vyake vitaishawishi Fifa kutupa uanachama,” alisema Attai.
Xxxxxx
Vodacom yadhamini Challenge kwa Mil 190
Na Mohamed Mharizo
KAMPUNI ya Simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imejitosa kudhamini Michuano ya Tusker Challenge kwa kutoa Sh milioni 190.
Vodacom inaungana na Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL) ambao ni wadhamini wakuu wa michuano hiyo kupitia bia ya Tusker waliowekeza Sh milioni 675.
Akizungumza katika makabidhiano yaliyofanyika Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Dar es Salaam jana, Mkuu wa Udhamini wa Vodacom, George Rwehumbiza alisema lengo lao ni kusaidia michuano yaweze kufana.
“Tunawashukuru TFF (Shirikisho la Soka Tanzania), CECAFA ( Baraza la Vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati na Tusker kwa kukubali nasi kushiriki kudhamini michuano hii, naamini tutashirikiana ili yawe bora hii”, alisema.
Alisema Vodacom itaendelea kushirikiana na TFF kukuza soka nchini na pia alitumia fursa hiyo kuzitakia kila la kheri timu za Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes.
Naye Rais wa CECAFA, Leodger Tenga aliwashukuru Vodacom kwa kukubali kushirikina na Tusker kudhamini michuano hiyo.
“Vodacom wamesikia kilio chetu, kwani tumekuwa tukiomba wadhamini zaidi kufanikisha michuano hii, pia niwashukuru Tusker kwa kukubali kuwa na Vodacom”, alisema.
Naye Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye naye aliwashukuru Vodacom kwa kuwa sehemu ya wadhamini wa michuano hiyo.
“Sisi CECAFA tunahitaji wadhamini wengi kuendesha michauno hii, tunashukuru Tusker pia kwa kuruhusu kusaka wadhamini wengine, matarajio yetu ni kufanikiwa zaidi,” alisema.
XxxxxMWISHO
AY kupamba usiku wa Miller leo Sun Cirro
Na Rachel Mwilligwa
MSANII wa bongo fleva nchini Ambwene Yesaya ‘A.Y’ leo atakuwa miongoni mwa wasanii watakaotoa burudani katika usiku maalum Miller Genuine Fresh.
Mbali ya A.Y, pia kundi la Kode Reds Djs kutoka nchini Kenya nao watafanya vitu vyao kuhakikisha mashabiki na wadau wa kinywaji hicho wanapata burudani ya uhakika.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, meneja wa bia hiyo, Victoria Kimaro burudani hiyo ni maalum kwa wateja wao ambao huo ni uzinduzi wa mpango mzima wa mwaka ujao na kwa kuanzia unazinduliwa leo klabu Sun Cirro kabla ya kupelekwa mikoani baadaye.
“Huu ni usiku maalum kwa wateja wa bia yetu ya Miller, ni usiku ambao mbali ya wateja hawa kupata burudani ikiwa ni kuwashukuru kwa kutuunga mkono mwaka mzima.
“Pia tutawasaka mabalozi wa bia hii watakaotambulika kama ‘VIP Miller’ ambao hawa ndio watakuwa mabalozi kwa mwaka mzima watakaojipatia fursa ya kuhudhuria shughuli mbalimbali za Miller ikiwapo kupewa bia hii kila mwezi pamoja na zawadi kama mabegi, fulana, kofia nk,” alisema Victoria.
Takribani wateja 250 wataingia bure kupitia kadi zao ambazo walijishindia kupitia promosheni za kinywaji hicho zilizokuwa zikipendwa huku kwa watakaoguswa na kutaka kushuhudia usiku huo watalipa Sh 10,000.
xxxxxxxxxxMWISHO

Post a Comment