Habari za Tanga
Na Oscar Assenga
Nipigra FC yaichapa Pangarawe FC 4-2
TIMU ya soka ya Nipigra FC juzi iliichapa timu ya Pangarawe FC mabao 4-2 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Pangarawe, Gombero wilayani Mkinga.
Nipigra walianza kuandika bao la kwanza dakika ya 25 kupitia kwa Salim Mwangesa kabla ya Jumaa Bakari kupachika bao la pili dakika ya 27.
Kuingia kwa mabao hayo kulisababisha Pangarawe FC kucharuka na dakika ya 30, Athuman Kwiru aliipatia timu yake bao la kwanza huku bao la pili likiwekwa nyavuni na Mgonja Bakari dakika ya 36.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu, hata hivyo Nipigra FC walifanikiwa kupachika bao la tatu dakika ya 48 lililofungwa na Omari Mwangena.
Dakika ya 86 ya mchezo huo, Riziki Salim aliwainua mashabiki wa timu ya Nipigra baada ya kuifungia timu yake bao la nne.
XxxxxMWISHO
Timu ya sheria yatamba kugawa dozi
KOCHA Mkuu wa timu ya Sheria Arogastian Kinindu ametamba kuendeleza dozi katika michuano ya Ligi ya Polisi inayoendelea katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majani Mapana.
Akizungumza na Mtanzania, Kinindu alisema kutokana na maandalizi mazuri ambayo timu yake imefanya, wana matumaini ya kuibuka na ushindi katika michuano hiyo ambayo mwaka huu inaonekana kuwa na msisimuko wa hali ya juu.
Timu hiyo ambayo ilikuwa tishio katika michuano iliyopita, imetamba kuendelea kugawa dozi kama kawaida yake.
Akihudhuria moja kati ya mapambano ya timu hiyo, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Liberatus Sabas aliwataka
Wachezaji, kuzingatia nidhamu katika michuano hiyo na kuwaeleza kuwa michezo ni ajira na moja ya kujitangaza hivyo hawana budi kujituma na kucheza kwa bidii ili kuweza kuibuka na ushindi.
XxxxxxxMWISHO
Nne zafuzu robo fainali Mkinga
TIMU nne zimefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya Mbagos Cup.
Akizungumza na Mtanzania, mratibu wa ligi hiyo, Kudura Kazadi alisema timu ambazo zimefuzu kuingia hatua hiyo ni nzuri hivyo kutakuwa na ushindani wa hali ya juu.
Kazadi alizitaja timu hizo ni Gurudumu FC, Express FC, Mazola FC, Bonivita na Nyundo FC. Aidha alizitaka timu hizo kuonyesha nidhamu ya hali ya juu katika hatua hiyo ili mshindi kupatikana kihalali bila manung’uniko.
Ligi hiyo ambayo ilianza hivi karibuni inaonekana kuwa kivutio kwa wadau mbalimbali wa soka wilayani Mkinga mkoani, Tanga.
XXXXXXXMWISHO
Salim: Nitawaunganisha waamuzi nchini
MGOMBEA nafasi ya uwakilishi katika Mkutano Mkuu wa (FRAT) Taifa kutoka Mkoa wa Tanga, Salim Juma amesema lengo la kugombea nafasi hiyo ni kutaka kuunganisha vyama vya waamuzi hapa nchini.
Akizungumza na Mtanzania, Juma alisema licha ya kuunganisha vyama vya waamuzi pia anatarajiwa kuleta mapinduzi ya kimaendeleo kwa waamuzi kwa kutumia busara za waamuzi waliopita ambao walikuwa ni mfano katika mkoa wa Tanga na taifa kwa ujumla.
Alisema atatumia mbinu mbalimbali za uongozi wa mpira na uamuzi ambao aliupata katika Chuo cha Michezo cha Kijeshi kilichopo Mgulani jijini Dar es Salaam.
“Nitatumia busara za waamuzi waliokuwa na uelewa mkubwa ili kuweza kuleta maendeleo katika chama hicho kama ilivyo kwa waamuzi waliopo mkoani hapa,” alisema Juma.
Aliwaomba waamuzi waliopo mkoani hapa kujitokeza kwa wingi ili kumpatia kura aweze kuleta maendeleo katika tasnia ya uamuzi kuanzia ngazi ya wilaya mkoa na taifa kwa ujumla.
XXXXXXmwisho.
Maveterani Tanga, Dar waungana
WACHEZAJI wa zamani waliowahi kucheza klabu mbalimbali za soka nchini pamoja na timu ya Taifa kutoka mkoa wa Tanga na Dar es Salaam, wameanzisha utaratibu wa kufanya mazoezi ya pamoja kila mwishoni mwa wiki.
Uamuzi huo una lengo la kuwaweka fiti na kujiimarisha miili yao ili kuweza kuepuka magonjwa yatokanayo na matumizi mabaya ya vyakula.
Mazoezi hayo ambayo yalianza kufanywa katika wilaya za Korogwe na Tanga kwa michezo ya riadha na mpira wa miguu yamewasaidia kwa kiasi kikubwa baadhi ya wachezaji waliotamba katika medani ya soka na wameweza kuunda timu zao kwa ajili ya kushiriki ligi ya Taifa.
Wakizungumza na Mtanzania katika viwanja vya Gymkhana jijini Tanga wakati wakipimana nguvu, viongozi wa klabu ya Namanga kutoka Dar es Salaam walisema lengo ni kuhakikisha miili yao inaimarika ili kuepukana na magonjwa pamoja na kuanzisha michezo ya wakongwe wa soka waliovuma hapa nchini.
Kwa upande wa akina mama Katibu Msaidizi wa Namanga Mary Joseph alisema utaratibu huo utawasaidia sana akina mama kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa
XXXXXXmwisho
Wadau wa ngumi wapewa somo
Na Kambi Mbwana
MDAU wa mchezo wa ngumi ambaye pia ni kocha wa Ashanti Boxing Club, Rajabu Mhamila ‘Super D’ amewataka wadau wa mchezo huo kufanya jitihada kuhakikisha unapata mafanikio.
Akizungumza na Mtanzania hivi karibuni, Super D alisema ngumi ni mchezo mzuri unaoweza kutoa ajira kwa wanamichezo wanaojihusisha nao kama ilivyo kwa mataifa makubwa Duniani licha ya Tanzania kuupa kisogo.
Alisema siku za nyuma wengi waliocheza ngumi waliweza kujiwekea mazingira mazuri kimaisha, sambamba na kupata nafasi ya kutembelea nchi mbalimbali kwa ajili ya masumbwi.
“Ipo haja ya wadau na wanamichezo wenyewe kuungana kwa pamoja ili kuhakikisha mchezo wa ngumi unakwenda mbele zaidi, ” alisema.
Ashanti Boxing Club imeanzishwa hivi karibuni ikiwa ni juhudi za wadau wa mchezo huo kuweka mikakati ya kuleta ari kwa vijana wanaopenda kujihusisha na masumbwi.
XxxxxMWISHO
Diamond kutimkia Nigeria
Na Jennifer Ullembo
MWIMBAJI wa bongo fleva nchini Nassib Juma ‘Diamond’ anatarajia kuondoka leo kuelekea nchini Nigeria kushiriki shindano la utoaji wa tuzo za muziki za MTV.
Akizungumza jana na Mtanzania Diamond aliwaomba mashabiki wake nchini kumpigia kura ili aweze kuibuka na ushindi katika tuzo hizo.
Alisema baada ya utoaji wa tuzo hizo kumalizika atarejea nchini Desemba 12 mwaka huu.
“Naomba nifike salama niweze kushuhudia mtanange huo maana si unajua wanaoshindanishwa kule wasanii wengi wenye vipaji,”alisema Diamond.
Aliongeza baada ya kurejea nchini anatarajia kurekodi video ya wimbo wake ujulikanao kama nitarejea unao patikana katika albamu yake ya nenda kamwambie .
Diamond ni mmoja wa wasanii wanaowania tuzo katika shindano hilo la utoaji tuzo za muziki litakalo fanyika nchini Nigeria Desemba 11 mwaka huu.
xxxxxxxxMWISHO

Post a Comment