Kagera mabingwa wa kupiga kasia
Na Rachel Mwilligwa
TIMU ya mkoa wa Kagera imeibuka mabingwa wa mwaka huu wa michuano ya kupiga kasia (Mbio za mitumbwi) zilizomalizika mwishoni mwa wiki.
Kagera, iliyowakilishwa na timu tatu za wanaume mbili na moja ya wanawake kama ilivyokuwa mikoa mingine, iliweka rekodi ya kuchukua ubingwa nafasi ya kwanza kwa upande wa wanaume na wanawake.
Mashindano hayo yaliyoanza kujizolea umaarufu hasa mikoa ya kanda ya ziwa, yalishirikisha jumla ya timu 18; na kati yake saba zilikuwa ni timu za wanawake.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Kanali Mlengo, alipongeza watengenezaji wa Bia ya Balimi kwa kudhamini mashindano hayo ambayo alisema yamechangia kuleta umoja kwa wakazi wa kanda ya ziwa.
Awali akizungumzia bia yake kudhamini mashindano hayo, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja alisema lengo lao ni kuukuza mchezo huo na kadri miaka inavyokwenda wamepania kuyaboresha zaidi.
“Tumepata mafanikio makubwa sana tangu tuanze mashindano haya miaka 12 iliyopita na azma yetu ni kuyaboresha zaidi kadri inavyowezekana, ” alisema Minja.
xxxxxxxMWISHO
Matumla: Pambano la Cheka, Maugo si mchezo
Na Kambi Mbwana
BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Mbwana Matumla, amesema pambano kati ya Francis Cheka na Mada Maugo litakuwa gumu na kutoa mshindi wa kweli kutokana na maandalizi na mikakati ya kila bondia.
Pambano hilo linatarajiwa kufanyika Januari Mosi mwakani, katika Ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam, huku likiwa na mvuto wa aina yake kutokana na vita ya maneno inayoendelea kwa mabondia hao.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Matumla alisema yoyote anaweza kuibuka na ushindi katika pambano hilo endapo atakuwa na ufundi wa kurusha masumbwi na umakini wa kucheza kwa mpinzani wake.
“Huwezi kutabiri kwa haraka nani anaweza kuwa juu kuliko mwenzake maana wote ni wazuri na wana uwezo wa kucheza ngumi kwa mafanikio tangu walipojiingiza katika fani hiyo,” alisema Matumla.
XxxxxxxMWISHO
Jaba Pool yaandaa bonanza
Na Mohamed Mharizo
KLABU ya mchezo wa Pool Table ya Jaba iliyopo Mwananyamala jijini, imeandaa bonanza kwa ajili ya kujipongeza kwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Taifa ya mchezo huo.
Bonanza hilo litafanyika Makao Makuu ya klabu hiyo kwa kuzikutanisha timu nyingine za wilaya hiyo na kushindana katika mchezo huo kwa klabu na wachezaji kucheza single single.
Mbali ya kujipongeza wenyewe, pia bonanza hilo litakuwa maalum kwa ajili ya kuipongeza timu ya Mkoa wa Kinondoni iliyotwaa ubingwa wa michuano hiyo ya Taifa iliyomalizika Arusha hivi karibuni.
Akizungumza na Mtanzania, Katibu Mkuu wa Jaba Michael Machellah alisema mshindi wa kwanza atajinyakulia Sh 50, 000, mshindi wa pili Sh 30, 000, wa tatu Sh 15, 000 na wa nne Sh 5, 000.
“Hii ni mara ya kwanza kwa klabu yetu (Jaba) kushiriki michuano hii, hivyo hatua tuliyofikia ni nzuri sana ndio maana tumeandaa bonanza hili,” alisema Machellah.
Alisema bonanza hilo linatarajia kushirikisha takribani wachezaji 120.
XXXXXMWISHO
Hardmad kuzindua imebaki stori
Na Edson Joel
MSANII wa muziki wa bongo fleva, Kidume Mnonji ‘Hardmad’anatarajia kuzindua albamu yake ya tatu itakayojulikana kama imebaki stori Desemba 10 katika ukumbi wa makumbusho ya Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Hardmad alisema albamu hiyo ina jumla ya nyimbo 11 ambazo zimeimbwa katika mahadhi tofauti.
Alitaja baadhi ya nyimbo zilizomo katika albamu hiyo ni Mtenda haki, Maono, Tupa mwili, Umesema unanipenda na Imebaki stori ambayo ndiyo iliyobeba jina la albamu hiyo.
“Ninaendelea na maandalizi taratibu ili Ijumaa nionyeshe nina uwezo mkubwa wa kuimba hususani sehemu za jukwaani,”alisema.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Maisha Music ambao ndiyo mdhamini na mwandaaji wa uzinduzi huo Kwame Mchauru alisema baada ya uzinduzi huo baadhi ya nyimbo zitafanyiwa video ili kutoa maana halisi ya kila wimbo husika.
xxxxMWISHO

Post a Comment