ad

ad

Kombe la Kiwangwa kuanza mwezi ujao

Na Patrick Mwillongo,Bagamoyo

KOMBE la Diwani wa kata ya Kiwangwa ambalo linashirikisha timu kutoka vijiji mbalimbali katika kata ya Kiwangwa inatarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.

Akizungumza na gazeti hili,Diwani wa kata ya Kiwangwa Makamba Shaaban,alisema kuwa michuano hiyo ambayo ina lengo la kuinua vipaji vya vijana wanamichezo katika kata hiyo.

“Ni kweli kama unavyojua kuwa serikali yetu imekuwa ikipigania kuinua sekta ya michezo nami pia nauunga mkono kwani niliahidi katika ahadi zangu za uchaguzi kuwa nitaanzisha michezo kwa ajili vijana lakini pia lengo hasa ni kuinua vipaji vipya”alisema.

Alisema kuwa kwa muda mrefu sasa michezo katika kata ya Kiwangwa imekuwa nyuma kutokana na vijana kushindwa kupata sehemu ya kuonyesha vipaji vyao hali ambayo ilikua ikichangia vijana wengi kuwa wazururaji na hatimaye kujiingiza katika ushawishi wa vitendo viovu.
Alisema kuwa mshindi wa kata ya Kiwangwa atakutana na mshindi wa kata ya Fukayosi ambapo timu itayoibuka na ushindi itaondoka na zawadi ya pikipiki na mshindi wa pili atajipatia fedha taslimu
Xxxxxxxxxxx
KAMATI ya mashindano ya chama cha mpira wa miguu wilayani Bagamoyo imezionya timu mbalimbali zilizopo wilayani kucha kufanya vitendo vya fujo na kuwaonya mashabiki wao kuachana na tabia ya kuanzisha vurugu

Akizungumza na gazeti hili katibu msaidizi Mzee Minjoli alisema kuwa kamati hiyo imeamua kutoa onyo kufuatia vurugu ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara katika michezo inayoendelea ya ligi ya taifa ya ngazi ya wilaya.

“Suala la vurugu kwa mashabiki na viongozi wa timu mbalimbali wilayani Bagamoyo limeanza kuwa sugu kwani karibu michezo inayofanyika katika uwanja wa Mwanakalenge imekuwa ikiisha kabla ya wakati kutokana na vurugu mbalimbali zinazoendelea kutoka kwa mashabiki,viongozi na wachezaji”alisema Minjoli.

Alisema kuwa katika kikao cha kamati hiyo kilichoketi Juzi,kamati ya mashindano imeamua kumfungia miezi 6 na faini ya shilingi 50,000,mchezaji Ally Bedi wa timu ya Super Star ‘Nyongolota’kutokana kwa kosa la kumshambulia mwamuzi Omary Hassan katika mchezo baina ya timu hiyo na Bafanabafana.

Aidha kamati hiyo pia imeitoza faini ya shilingi laki moja timu hiyo kwa kosa la mashabiki wake kumshambulia mwamuzi Omary Hassan na kuongeza kuwa kamati hiyo inataraji kuketi hivi karibuni kwa ajili ya kuangalia namna itavyoweza kudhibiti vitendo vya vurugu katika uwanja wa Mwanakelenge.
Xxxxxxxxxxx
TIMU ya mpira wa miguu ya wanawake ya Bagamoyo queens inajiandaa kucheza michezo mbalimbali ya kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya soka kwa wanawake mkoa wa Pwani.

Akizungumza na gazeti hili Kocha Mkuu wa timu hiyo Kunjumu Omary alisema kuwa michezo hiyo itawasaidia wachezaji wake ambao wengi wao wanasoma katika shule ya vipaji ya Lord Barden Power.

“Michezo hii itasaidia sana wachezaji wangu katika kujiandaa na michuano ya soka kwa wanawake kwa mkoa wa Pwani na pia kuwawezesha kukaa pamoja tena kwani kwa muda mrefu wengi walikuwa shuleni”alisema Kunjumu

Alisema timu yake ambayo ni moja ya timu tishio kwa upande wa soka la wanawake inataraji kucheza michezo hiyo ya kirafiki na timu za Msimbazi queens,Mburahati Queens,na shule za sekondari Makongo na Jitegemee.
Aidha Kunjumu aliwataka wadau mbalimbali kujitokeza kuisadia timu kwa hali na mali kwani mpaka sasa kikosi hicho knakabiliwa na tatizo la uhaba wa vifaa vya mazoezi na mechi na kusema kuwa ni matumaini yake wadau watajitokeza na kuisadia timu hiyo.
Xxxxxxxxxxxx
ASASI isiyo ya kiserikali ya Uhakika kituo cha Ushauri nasaha UKUN ya wilayani Bagamoyo imetoa msaada wa mipira ya soka kwa viongozi wa vijiji wilayani humo

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo,Mratibu wa mpango ‘WASH’Charles Njonjele alisema kuwa asasi yake imeamua kutoa mipira hiyo ili kushindaniwa na timu mbalimbali katika vijiji husika

“Napenda kuchukua fursa hiyo kuwakabidhi mipira hii ambayo imetolewa na asasi yangu kupitia mpango wa kunawa mikono kblaya kula,kunawa na kutoka chooni ‘WASH’ unaofadhiliwa na PSI na mipira hii imetolewa kwa vile vijiji ambavyo havina zahanati”alisema

Alisema kuwa wameamua kutoa mipira hiyo kwa vijiji ambavyo havina zahanati kwa kuwa michezo ni sehemu moja wapo inayokutanisha watu wengi hivyo kwa kufanya hivyo itachangia wahudumu wa afya ya msingi katika vijiji hivyo kutoa elimu ya unawaji mikono wakati michezo hiyo ikiwa inaendelea

Alisema kuwa mipira hiyo ambayo ina thamani ya zadi shilingi milioni moja itatumika katika michezo hiyo na itatolewa kama zawadi kwa washindi watakaokuwa wamepatikana wakati wa michezo hiyo.
Xxxxxxxxxx
LIGI ya soka ya Taifa ngazi ya wilaya imeendelea kurindima wilayani Bagamoyo ambapo katika mchezo uliofanyika juzi katika uwanja wa Mwanakalenge timu ya Majengo Stars iliifunga timu ya Mboya kwa mabao 3-0.

Aidha katika mchezo mwingine timu ya Alhadadi imeweza kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya timu ya Motodazo katika mchezo mkali ambao ulikuwa ni wa vuta nikuvute kwa timu zote mbili.

Katika mchezo uliochezwa jana timu ya Kaole Fc na Uswazi Fc zilitoshana nguvu baada ya kufungana bao 1-1 katika mchezo uliochezwa uliofanyika katika uwanja wa Mwanakalenge

Ligi ya Taifa ngazi ya wilaya,wilayani Bagamoyo inachezwa katika vituo viwili vya Mwanakalenge na shule ya sekondari ya Lugoba katika jimbo la Chalinze ambapo washindi wawili wa kila kituo watakutana na kutoa timu itayojiunga na ligi daraja la kwanza nchini.
Xxxxxxxx

KIROMO VIEW KUWAKA MOTO LEO
Na Patrick Mwillongo,Bagamoyo
JUMLA ya vijana 4500-6000 wanataraji kukutana leo katika hoteli ya kitalii ya Kiromo View katika tamasha maalum la kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa chuo cha fedha IFM

Akizungumza na gazeti hili Mkurugenzi wa hoteli ya Kiromo James Nickolaus Mujunangoma alisema tamasha hilo linalokwenda kwa jina la IFM Concert Bash’litawakutanisha wanafunzi mbalimbali

Mujunangoma alisema kuwa tamasha hilo litakuwa na michezo na burudani mbalimbali ikiwamo muziki wa kizazi kipya,disco na kuwa kutakuwa burudani ya ngoma za asili

“Kwa ukweli tumejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa tamasha hilo linafanikiwa kwani kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwamo muziki wa kizazi kipya,muziki wa Dansi na ngoma za asili ni tamasha ambalo kiuhakika litafana sana”

Alisema kuwa pamoja na kutoa huduma za hoteli,Kiromo pia imekuwa ikidhamini matamasha mbalimbali na hivi karibuni imeweza kudhamini kambi ya warembo wa Miss Utalii kwa jumla ya shilingi 150 milioni.

No comments