‘Kilimanjaro Stars ushindi lazima’
Na Rachel Mwilligwa
TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, leo inashuka dimbani kumenyana na Burundi katika mfululizo wa michuano ya Kombe la Challenge inayoendelea jijini.
Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini, utakuwa mgumu kwa pande zote hasa kwa Kili Stars inayohitaji kushinda.
Hilo halina ubishi, ndio unaweza kusema ushindi ni lazima kwa Kili Stars leo ili iweze kusonga mbele katika michuano hiyo na kufuta aibu ya wenyeji kuondolewa mapema.
Hiyo ni kutokana na Kili Stars kujikusanyia pointi tatu kutoka mechi mbili ilizocheza baada ya kushindwa mchezo mmoja na kupoteza mmoja.
Ilipoteza ilipokubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Zambia kabla ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Somalia.
Hakuna ubishi Kili inahitaji kujirekebisha mno katika safu yake ya ushambuliaji na kiungo ambayo imekuwa ni tatizo sugu linalohitaji kupatiwa ufumbuzi ambao ni muhimu ufumbuzi huo uanze kusakwa katika mchezo wa leo.
Akizungumza baada ya kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Zambia huo ukiwa ni mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo Jumamosi iliyopita (Novemba 27), Kocha Mkuu wa Kili Stars, Jan Poulsen alisema.
“Nina matatizo makubwa kwenye nafasi ya kiungo na ushambuliaji ambayo nimeishayafanyia kazi naomba mashabiki wawe na matumaini tutafanya vizuri,” alisema Poulsen.
Katika hatua nyingine, timu ya Taifa ya Zambia iliendeleza ubabe baada ya kuibamiza Somalia 6-0.
MWISHO
Harambee Stars wajitoa Challenge
Na Deborah Kajolo
TIMU ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ imejitoa kuendelea kushiriki michuano ya Kombe la Challenge inayoendelea jijini.
Kikosi hicho cha wachezaji 20 kimegomea mchezo wa kesho dhidi ya mabingwa watetezi kwenye michuano hiyo Uganda ‘The Cranes’.
Uamuzi huo umekuja baada ya Harambee kudai posho kutoka Shirikisho la Soka la Kenya (KFF) tangu walipokuja nchini kushiriki michuano hii ya CECAFA.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kocha mkuu wa timu hiyo, Jacob ‘Ghost’ Mulee alisema ameaamua kuweka hadharani hilo ili wadau waweze kujua sababu ya wachezaji wake kukataa kucheza mechi hiyo ni posho hizo ambazo hawajui watalipwa lini na Shirikisho la Soka la Kenya (KFF).
Alisema KFF iliahidi kuwapa fedha hizo, Jumanne na baadaye juzi, Alhamisi kabla ya mechi yao na Ethiopia waliahidiwa kupewa fedha hizo na sasa ni Ijumaa ‘jana’ lakini hamna dalili yeyote ya kulipwa.
“Sina la kufanya, kama ni jipu limeshapasuka, kwani ni siku ya 19 sasa wachezaji na viongozi watano tunadai posho kwani hawajatulipa tangu tulipoanza mazoezi ya kujiandaa na michuano hii ingawa siwezi kutaja kiasi tunachodai lakini naomba tueleweke kuwa sababu si kuogopa Uganda,” alisema Mulee.
Kocha huyo alisema hakuna anachoweza kufanya kwani hilo limeamuliwa na wachezaji, hivyo hawezi kuwalazimisha kwa lolote pamoja na kujua umuhimu wa mechi hiyo na kuwa siku yeyote watakayotakiwa kurudi Kenya wapo tayari kwani wameshajiandaa.
Naye nahodha wa Harambee Stars, James Situma alisema maamuzi ya kutocheza mechi hiyo si shinikizo la mtu yeyote ila ni wachezaji wenyewe kwani wameona ni uonevu na ubabaishaji mkubwa unaendelea wakati wanajua kabisa kuwa na wao wana mahitaji muhimu.
xxxxxxxxxMWISHO

Post a Comment