Mrithi wa Mwakalebela huyu hapa
Na Mwandishi Wetu
HATIMAYE Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limepata Katibu Mkuu wake, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Fredreck Mwakalebela aliyemaliza muda wake Julai mwaka huu.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana, aliyefanikiwa kutwaa nafasi hiyo ni mwandishi wa siku nyingi wa michezo, Angetile Osiah, huku Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, Boniphace Wambura akiikwaa nafasi ya Ofisa Habari wa shirikisho hilo.
Awali, nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Florian Kaijage aliyetimuliwa kwa kile kilichoolezwa kuwa ni kutokana na uzembe.
Mbali na wawili hao, mwingine aliyefanikiwa kuula TFF ni mtangazaji wa siku nyingi wa redio na TV, Jimmy Kabwe anachukua nafasi ya Ofisa Masoko wa shirikisho hilo. Nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Daniel Msangi.
Habari zaidi zilidai kuwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga, alitarajiwa kuwatangaza watatu hao jana baada ya mchezo wa fainali ya Kombe la Challenge kati ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ na Ivory Coast kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
xxxxxxxxMWISHO

Post a Comment