ad

ad

TAMASHA LA STR8 MUSIC MORO LAFANA

Msanii wa nyimbo za kizazi kipya Dar. S.Tamina akifanya vitu vyake jukwani wakati wa onyesho hilo.
Msanii Mangwea akichana mistari jukwani wakati wa onyesho hilo
Msanii Richie Mavocal akifunga pazia la onyesho hilo.
Mwana FA, Fid Q wapagawisha Str8Muzik
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
WASANII wa muziki wa kizazi kipya, Mwinjuma Hamisi maarufu kama Mwana
FA na Fareed Kubanda aka Fid Q, walikuwa kivutio kwa mashabiki wa
muziki waliojitokeza kwa wingi juzi katika viwanja vya Magadu mkoani
Morogoro kwenye tamasha la Str8Muzik.

Tamasha hili ambalo hufanyika kila mwaka na kuwakutanisha wanafunzi wa
vyuo vikuu na elimu ya juu pamoja na mashabiki wa muziki hudhaminiwa
na Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) kupitia chapa yake ya Sweet
Menthol (SM).

Fid Q alikonga nyoyo za mashabiki wengi kwa nyimbo zake za zamani na
pia jambo lililomfanya arudi stejini zaidi ya mara moja. Miongoni mwa
nyimbo zake zilizowavutia mashabiki wa muziki ni ‘Mwanza Mwanza’,
‘Kiubishi Ubishi’ na ‘Chagua Moja’.

Msanii huyu ambaye amejizoelea umaarufu kwote nchini, aliwaomba radhi
mashabiki wake ambao walitaka aimbe wimbo wa ‘Propaganda’ akisema kuwa
hakuja na ala za muziki huyo ila akawaridhisha kwa kuwapa mashairi ya
wimbo huo.

Mwana FA aka Binamu naye pia alikuwa kipenzi cha mashabiki wengi
waliyohudhuria tamasha hilo na aliimba nyimbo zake kwa pamoja na umati
mkubwa uliyohudhuria.

Miongoni mwa nyimbo za Mwana FA zilizokonga mashabiki wa muziki ni
‘Alikufa kwa Ngoma’, ‘Naongea na Wewe’, ‘Mabinti’ na ‘Bado Nipo Nipo’.

Aidha msanii huyu pia aliimba nyimbo zingine kama vile ‘Usije Mjini’,
‘Msiache Kuongea’, ‘Unanitega’, ‘Dakika Moja’ na ‘Habari Ndo Hiyo’.

Msanii mwalikwa kutoka Uganda, Michael Ross, kabla ya kupanda jukwani
aliimbiwa wimbo wa ‘Happy Birthday’ kama ishara ya kuadhimisha siku
yake ya kuzaliwa na wasanii wote waliyotumbuiza usiku wa kuamikia jana
usiku pamoja na umati uliyohudhuria tamasha la Str8Muzik.

Michael Ross alisema amefarijika kualikwa tena katika tamasha la
Str8Muzik na jinsi gani mashabiki wake hususan wanafunzi wanavyokubali
nyimbo zake.

“Hii ni heshima kubwa kuja kwa mara nyingine kutumbuiza katika tamasha
hili linalowaleta wanafunzi wa vyuo vikuu na elimu ya juu kuja
kuburudika na kubadilisha mawazo,” alisema msanii huyo kutoka Uganda.

Mwana FA naye aliongeza kusema kuwa tamasha la juzi limefanikiwa kwa
kiasi kikubwa kwasababu idadi ya watu ambao wengi wao walikuwa
wanafunzi walijitokeza kwa wingi.

Wasanii wengine ambao walitumbiza na kuwapagawisha mashabiki
waliyohudhuria tamasha hilo ni Joh Makini, Mangwea, Nicky Mavocal
anayetamba na nyimbo yake ‘Nibembeleza kwa guitar’ na Shatta kutoka
Ilala, Dar es Salaam.
Fid Q
Wanachuo wa Mzumbe na Sokoine wakichuana katika free style
Michael Rossi kutika Uganda akiimba
Michael Rossi akifanya vitu vyake

No comments