TAMASHA LA ZANTEL EAST AFRICAN BASH-DAR WEST.
AY, Amani, Ngoni wapagawisha Zantel East African Bash
Na mohamed mharizo
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva katika Ukanda wa Afrika Mashariki juzi walitoa burudani katika Tamasha la East African Bash na kuwaleta pamoja wateja wa Zantel.
Tamasha hilo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Dar West Park Tabata, Dar es Salaam, ambapo msanii Ambwene Yessayah, ‘AY’ (Tanzania), Cecilia Wairimu, ‘Amani’ kundi la Ngoni kutoka Uganda likiongozwa na Aydee Dumba na Pato Nyanzi.
Lengo la tamasha hilo ni kuwaunganisha wasanii ikiwa ni jitihada za wanasiasa kuelekea Shirikisho la Afrika Mashariki.
Baadhi ya nyimbo alizoimba AY ni pamoja na Machoni kama watu, Ni raha tu, Binadamu, Yule, Sitomwacha, Hii leo, Usije mjini na Habari ndio hii.
Kwa upande wa Amani aliimba nyimbo za Songa karibu, Utaipenda, Missing my baby na Tonight.
Msanii huyo wa kike mara baada ya kushuka jukwaani alisema anajisikia faraja kupata mialiko mingi nchini Tanzania na hiyo inampa faraja kuwa nyimbo zake zinapendwa.
Kwa upande wa Ngoni walipanda jukwaani na kuimba nyimbo za Bigula, Mimi na Wewe, Ningoje na Nasilimagwe.
Tamasha hilo la siku mbili, lilitarajiwa kufikia tamati jana kwenye Ukumbi wa Mbalamwezi Beach Resort.
Tamasha hilo liliandaliwa na Giltz Entertainment na kudhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Channel Ten, Paradise Hotel na Air Uganda.
Post a Comment