AFC ARUSHA YAJINOA KUICHAPA MAJIMAJI SONGEA
KOCHA wa timu ya AFC ya Arusha,Wilfred Kidau ametamba kutoa kipigo kikali kwa timu ya Majimaji ya Songea kwennye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom inayotarajiwa kufanyika Septemba 22 mwaka kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Akizungumza na mwndishi wa Gazeti hili mjini Arusha Kidau alisema amejifunza mambo mengi na mbinu nyingiu kutokana na mechi tatu ambazo tayari ameshazicheza kwenye ligi hiyo.
Kidau alisema,tatizo kubwa lilikuwa ni upande wa umaliziaji ambapo mpaka sasa ameshaliweka sawa na makosa mengene madogo tayari yako safi na hivyo inampelekea kujiamini kufanya vizuri mechi hiyo na zingine zote zinazofuata.
AFC mpaka sasa imepoteza mechi tatu ambazo ni ya Azama walifungwa 2-0, ya Afrika Lyon walifungwa 1-0 na ya Yanga ambayo walifungwa 2-0.
Timu ya AFC inatarajiwa kuondoka jumapili kuelekea Songea na usafiri maalumu ambapo watalala mahala kati ya Morogoro au Njombe na jumanne kuwasili Songea
Kocha wa Mkuu timu ya AFC ya Arusha, Wilfred Kidau akiwaelekeza jambo wachezaji wakati wa mazoezi kwenye Uwanja wa General Tyer mjini Arusha jana
Timu 8 zatinga fainali Pool Safari Lager
TIMU nane za zinazowakilisha mikoa mbalimbali kwenye mashindano ya Kitaifa ya Pool Safari Lager zimefanikiwa kuingia robo fainali wakati timu sita zimeondolewa kwenye mashindano hayo.
Timu zlizofanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ni Kinondoni,Ilala,Temeke,Dodoma,Morogoro,Iringa,Mbeya na wenyeji wa mashindano hayo Arusha.
Timu zilizoyaaga mashindano hayo ni Mwanza,Shinyanga,Kagera,Manyala,Tanga,na Bukoba.
Ushindani umekuwa ni wahali ya juu
Toka mashindano yaanze mpaka sasa kunawachezaji ambao wametengeneza rekodi binafsi ambao ni Festo Yohana wa kitoka Mkoa wa kimchezo wa Ilala na Amiri Ngayana kutoka Temeke wana A,kila mmoja ambayo mchezaji huipata kwa kuanza kucheza na kumaliza mchezo bila mpinzani kucheza.
Fainali za mashindano hayo zinatarajiwa kumalizika leo mjini Arusha na Mgeni rasmi atakaefunga mashindano hayo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Isdory Shirima.
Post a Comment