ad

ad

FAINLI ZA POOL SAFARI LAGER ZAENDELEA ARUSHA

AWaandishi wa habari wa michezo,kutoka kushoto ni Alex Lwambano wa Radio Claus,Jane John wa TBC na Rajabu Mwamila wa Majira wakiwajibika Kaunter.
Wakitazama picha
Refa akisawazisha mambo kwa wachezaji wakati wa mashindano ya Safari Lager
Mashabiki wakishangilia
Mchezaji wa Ilala akicheza

Wasanii nao hawako nyuma katika kutoa burudani kama hivyo

Wachezaji mmoja mmoja upande wa kike wakicheza,Shamira Mohamed kutoka Mwanza (kushoto) na Cecilia Kileo kutoka Kilimanjaro
Cecilia akicheza
Shamira akicheza
Madina Idd kutoka Temeke akicheza
Happy Ngumbo kutoka Dodoma akicheza
Betty Sanga kutoka Mbeya akicheza
Wachezaji wakisaini mara baada ya mchezo kumalizika

ILALA YAANZA VYEMA

MABINGWA watetezi wa mashindano ya Pool Safari Lager Ilala wameanza kwa kishindo kwenye ufunguzi wa mashindano yaliyoanza juzi mjini Arusha huku Kinondoni wakiwanyemelea wakti Temeke yenyewe iliyanza vibaya mashindano hayo.

Temeke ilianza vibaya fainali hizo zinazodhaminiwa na bia ya Safari Lager baada ya kupata kipigo cha magoli 14-11 kutoka mkoa wa Mwanza, mabingwa watetezi, Ilala yenyewe ilianza vema kutetea ubingwa wake baada ya kuichapa Iringa magoli 15-10.

Mkoa maalum wa kimichezo wa Kinondoni nao ulianza vema fainali hizo baada ya kuikandamiza Marogoro magoli 17-8, huku wenyeji wa mashindano hayo, Arusha ikijihakikishia kucheza robo fainali kufuatia kushinda michezo yake miwili dhidi ya Manyara na Mbeya kwa kuibuka na ushindi wa magoli 16-9 kwa kila mchezo.

Wageni wa mashindano hayo mikoa ya Kagera na Shinyanga ambayo imeanza kushirikia mashindano hayo kwa mara kwanza mwaka huu, ikianza vibaya mashindano hayo.

Mkoa wa Kagera ulibanjuliwa magoli 17-8 na Tanga na Shinyanga ikilala kwa magoli magoli 18-7 kutoka mkoa wa Morogoro, nao mkoa wa Dodoma ulijiweka katika mazingira mazuri ya kucheza robo fainali baada ya kushinda michezo yake miwili dhidi ya Tanga na Iringa ambapo iliifunga Iringa magoli 13-12 na ikaichapa Tanga 18-7, katika mchezo mwingine Mbeya iliichapa Kilimanjaro magoli 16-9.

Mashindano hayo yanatarajia kumalizika kesho kwa bingwa kuondoka na fedha taslim Sh.3,500,000 kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo bia ya Safari Lager.

Mashindano hayo yatafungwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdory Shirima ambaye ndiye atakayekuwa mgeni rasmi kwa kilele cha fainali hizo.

Beatrice Kabuku kutoka Kagera akicheza
Vailet Mrema kutoka Kinondoni akicheza
Leila Hussein kutoka Tanga akicheza
Majaliwa Haruna kutoka Kinondoni akicheza
Khalid Ahmed kutokaManyara akicheza




Wachezaji wakiweka sahihi

No comments