ad

ad

Bingwa Kujishindia milioni moja mashindano ya Ufukweni.

 Golikipa wa timu ya Dar Beach Fc, Amani Kajo akijaribu kokoa mpira dhidi ya timu ya Everything Fc wakati wa mechi ya  ufunguzi wa mashindano ya Beach Soccer Cleanup yanayoendelea katika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya usafi wa Bahari Duniani pamoja na kuunga mkono kampeni ya Serikali ya kuachana na matumizi ya mifuko ya Plastiki.Makampuni mbambali yalijitokeza leo kufanya usafi kati ufukwe wa Coco Beach yakiwemo Pepsi, RedBull, Slipway Hoteli, G1 Security Limited, AfyaPal(Muhimbili),Toshiba, Zenufa, HasafaScience, Verge Africa na Nipe Fagio.
 Mchezaji wa timu ya Everything, Nathanael Weiss akijiandaa kupiga tikitaka wakati golikipa akijiandaa pia kuzuia wakati wa mechi ya  ufunguzi wa mashindano ya Beach Soccer Cleanup yanayoendelea katika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya usafi wa Bahari Duniani pamoja na kuunga mkono kampeni ya Serikali ya kuachana na matumizi ya mifuko ya Plastiki.Makampuni mbambali yalijitokeza leo kufanya usafi kati ufukwe wa Coco Beach yakiwemo Pepsi, RedBull, Slipway Hoteli, G1 Security Limited, AfyaPal(Muhimbili),Toshiba, Zenufa, HasafaScience, Verge Africa na Nipe Fagio.

 Mchezaji wa timu ya Everything, Nathanael Weiss akijaribu kuwapenya kipa na beki wa Dar Beach Fc wakati wa mechi ya  ufunguzi wa mashindano ya Beach Soccer Cleanup yanayoendelea katika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya usafi wa Bahari Duniani pamoja na kuunga mkono kampeni ya Serikali ya kuachana na matumizi ya mifuko ya Plastiki.Makampuni mbambali yalijitokeza leo kufanya usafi kati ufukwe wa Coco Beach yakiwemo Pepsi, RedBull, Slipway Hoteli, G1 Security Limited, AfyaPal(Muhimbili),Toshiba, Zenufa, HasafaScience, Verge Africa na Nipe Fagio.

Na Mwandishi Wetu.
Bingwa Kujishindia milioni moja mashindano ya Ufukweni.
TIMU mbalimbali zimejitokeza kushiriki mashindano ya mpira wa miguu ya ufukweni katika kusherehekea siku ya Usafi wa Bahari Duniani pamoja na kuunga mkono Kampeni ya Serikari ya kutokomeza matumizi ya mifuko ya Plastiki.
Katika kuadhimisha siku hiyo Makampuni mbalimbali jijini Dar es Salaam yamefanya usafi ufukwe wa Coco Beach ambapo huadhimishwa Juni 8 kila mwaka.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwakilishi wa waratibu wa shughuli hiyo kutoka Kampuni ya Verge Africa, Hafsa Mambosasa alisema wao kwa kushirikiana na makampuni rafiki wameungana kufanya shughuli hii ya kijamii ikiwa ni sehema ya kuihamasisha jamii kuwa swala la kutunza mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu.
Mratibu Hafsa aliyataja makampuni yaliyojitokeza kuwa ni Kampuni ya vinywaji ya Pepsi, Red Bull, Hoteli ya Slipway, G1 Security Limited, AfyaPal(Muhimbili),  Toshiba, Zenufa, Hasafa Science  na Nipe Fagio.
Jumla ya timu 14 zimejitokeza kushiriki usafi wa Ufukwe wa Bahari pamoja na mashindano ya ufukwe ambazo ni Dar Beach Warmer, Every Living things, Safina Athletics, Mkude Fc, Osterbay City, JMK Fc, Beach Boys, CBE Combine, Samsal Fc, All Stars, We Kick Balls Fc, GEGE Fc, Gerezani Fc, Future Stars.
Hafsa alizitaja zawadi za washindi kuwa bingwa atajinyakulia pesa taslimu shilingi milioni moja, mshindi wa pili shilingi laki sita na mshindi wa tatu atapata vocha ya kwenda kufurahi katika Hoteli ya Slipway. 
Mchezaji wa timu ya Everything, Erasto Mwakilenge akimtoka mchezaji wa Dar Beach F, Ibrahimu Mussa wakati wa Fc wakati wa mechi ya  ufunguzi wa mashindano ya Beach Soccer Cleanup yanayoendelea katika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya usafi wa Bahari Duniani pamoja na kuunga mkono kampeni ya Serikali ya kuachana na matumizi ya mifuko ya Plastiki.Makampuni mbambali yalijitokeza leo kufanya usafi kati ufukwe wa Coco Beach yakiwemo Pepsi, RedBull, Slipway Hoteli, G1 Security Limited, AfyaPal(Muhimbili),Toshiba, Zenufa, HasafaScience, Verge Africa na Nipe Fagio.

No comments