‘TIMU 24, ZATINGA ROBO FAINALI CASTLE LAGER 5s’
Mchezaji wa
team Z,ya Ilala akijaribu kuwatoka wachezaji wa team Kiba wakati wa Bonanza la
Castle 5s(5-aside) lililofanyika Viwanja vya Sigara Tabata mwishoni mwa
wiki.Bingwa katika mashindano hayo ataiwakilisha inchi ya Tanzania katika mashindano
ya Afrika yanayotarajiwa kufanyka Zambia.
Mchezaji wa
team Kiba,ya Ilala akijaribu kuwatoka wachezaji wa team Simba wakati wa Bonanza
la Castle 5s(5-aside) lililofanyika Viwanja vya Sigara Tabata mwishoni mwa
wiki.Bingwa katika mashindano hayo ataiwakilisha inchi ya Tanzania katika
mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyka Zambia
Mchezaji
wa timu Kiba,ya Ilala akijaribu kufunga wakati wa mechi ya Bonanza dhidi ya timu
Simba wakati wa Bonanza la Castle 5s(5-aside) lililofanyika Viwanja vya Sigara
Tabata mwishoni mwa wiki.Bingwa katika mashindano hayo ataiwakilisha inchi ya
Tanzania katika mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyka Zambia
Wachezaji wa timu ya Kenge Bar ya Kimara wakipongezana mara baada ya kufanikiwa kuingia robo fainali wakati wa Bonanza la Castle Africa 5s(5- aside) lililofanyika Viwanja vya Kinesi Sinza Shekilango mwishoni mwa wiki. Bingwa katika mashindano hayo ataiwakilisha inchi ya Tanzania katika mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyka Zambia.
MASHINDANO ya soka ya “Castle Lager Africa 5s’ yalifanikiwa kuanza rasmi mwishoni mwa wiki ambapo timu 24 kutoka bar tofauti zimefanikiwa kuingia robo fainali jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya Kenge Bar ya Kimara wakipongezana mara baada ya kufanikiwa kuingia robo fainali wakati wa Bonanza la Castle Africa 5s(5- aside) lililofanyika Viwanja vya Kinesi Sinza Shekilango mwishoni mwa wiki. Bingwa katika mashindano hayo ataiwakilisha inchi ya Tanzania katika mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyka Zambia.
MASHINDANO ya soka ya “Castle Lager Africa 5s’ yalifanikiwa kuanza rasmi mwishoni mwa wiki ambapo timu 24 kutoka bar tofauti zimefanikiwa kuingia robo fainali jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo yalichezwa katika mfumo wa bonanza yaliandaliwa na
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia Bia yake ya Castle Lager. Kila timu itaundwa
na wachezaji watano (5) na mmoja wa akiba.
Ili kupata timu shiriki, wateja wanatakiwa kununua bia ya Castle Lager
kupitia katika promosheni mbalimbali zinazofanyika kwa nyakati tofauti katika
baa 160 za maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam. Kuna maeneo 10 tofauti
na kila eneo lina baa 16.
Mteja kutoka baa husika, atatakiwa kununua bia ya Castle Lager na baadaye
kupewa fomu maalumu ya kujaza ili kupendekeza majina ya wachezaji watano na
mmoja wa akiba, na hakuna kiingilio au malipo yoyote kwa timu kujisajili na kushiriki.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bia
ya Castle Lager, Pamela Kikuli, alisema kuwa, baada ya kupata timu katika
mchakato wa awali, kutakuwa na hatua nyingine ya upigaji wa kura kwa wateja wa
baa husika, ili kupata timu moja itakayowakilisha baa hiyo.
“Baada ya kupata timu zitakazokuwa zimefanikiwa kuwakilisha baa husika,
kutakuwa na bonanza maalumu ambapo timu 16 zitatoa timu nane (8) na baadaye
kupata timu moja itakayowakilisha kundi moja. Timu 10 zilizopatikana katika makundi zitacheza
katika bonanza kubwa litakalofanyika Aprili 28, 2018 katika Viwanja vya Leaders, jijini Dar es
Salaaam,” alisema Kikuli
Pamoja na soka, Kikuli alisema kuwa,
kutakuwa burudani ya muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali maarufu pamoja na
nyama choma na kuwa, michuano hii haitowahusisha wachezaji wanaoshiriki katika
ligi zozote za nje wala ndani.
Bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha
Tanzania katika michuano ya Afrika itakayofanyika Zambia. Endapo Tanzania
itashinda katika michuano hiyo, itapata fursa ya kwenda Urusi kushuhudia mechi mojawapo
ya Kombe la Dunia baadaye mwaka huu, ikiambatana na mashabiki wawili watakaopatikana
kwa kuchezesha bahati nasibu ya wanywaji wa Castle Lager.
Katika hatua nyingine, Kikuli alimtaja
mkongwe wa soka nchini, Ivo Mapunda kama balozi wa michuano hii ambaye
atahudhuria mabonanza hayo kwa nyakati
tofauti ili kutoa mafunzo kwa wachezaji.
Katika nyakati tofauti Mapunda aliwahi
kuzichezea timu za Prisons, Simba, Yanga na Timu ya soka ya taifa ‘Taifa Stars’
akiwa kama mlinda mlango.
Aidha ataifundisha timu ya Tanzania kabla ya
kwenda Zambia, na pia endapo Tanzania itashinda ataambatana na timu hiyo kwenda
Urusi kushuhudia Kombe la Dunia.
Timu za Afrika zitakashiriki katika
mashindano ya Kombe la Dunia itakayoanza kutimua vumbi Juni 14 hadi 25 mwaka
huu nchini Urusi ni Misri, Morocco,Tunisia, Nigeria na Senegal.
Wachezaji wa
timu Ushindi ya Ubungo wakipongezana mara baada ya kufanikiwa kuingia robo
fainali wakati wa Bonanza la Castle Africa 5s(5- aside) lililofanyika Viwanja
vya Kinesi Sinza Shekilango mwishoni mwa wiki. Bingwa katika mashindano hayo
ataiwakilisha inchi ya Tanzania katika mashindano ya Afrika yanayotarajiwa
kufanyka Zambia.
Post a Comment