Huawei, Clara Boutique wazindua duka kubwa Kanda ya Ziwa
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Huawei Tanzania,
Bruce Zhang(kulia) na Mkurugenzi wa Clara Huawei Smartphone Brand Shop, Clara
Mwasa wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Duka hilo uliofanyika mwishoni mwa
wiki jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu
wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Bruce
Zhang(kulia) ikiwapungia mkono wageni waalikwa mara baada ya uzinduzi wa duka
la Clara Huawei Smartphone Brand Shop lililoko jijini Mwanza.Kulia ni
Mkurugenzi wa Duka hilo, Clara Mwasa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Huawei Tanzania,
Bruce Zhang(katikati) akiwaonyesha wateja walihudhuria uzinduzi wa Duka la
Clara Huawei Smartphone Brand Shop
lililozinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.Kulia ni Mkurugenzi wa
Duka hilo, Clara Mwasa.
Huawei, Clara Boutique wazindua duka kubwa Kanda ya Ziwa
Kampuni ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Huawei
Tanzania kwa kushirikiana na Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, Clara Salon
& Boutique imefungua duka kubwa liitwalo “Clara Smartphone Shop” katika Jiji
la Mwanza. Hatua hiyo ni mwendelezo wa Huawei katika kutekeleza moja ya
mikakati yake ya kujitanua kibiashara nchini.
Huawei imeona kuwepo wa Duka hili kubwa la Clara, katika Jiji la Mwanza
kunatokana na kukua mahitaji ya bidhaa za Huawei nchini na hivyo kutoa fursa ya
watumiaji kupata huduma kwa karibu zaidi.
“Tunafahamu watanzania walio wengi wanachohitaji, ndiyo maana leo hii
tuko Mwanza. Tunaamini kuwa hii ni fursa pekee kwa wakazi wa Mwanza na miji ya
jirani kupata bidhaa zetu zenye ubora na viwango vya hali ya juu. Tunaamini
kuwa Clara Salon & Boutique wana jina kubwa katika Jiji la Mwanza na hivyo
itatusaidia sisi kutimiza lengo letu, anasema Mkurugenzi huyo.
Mwaka huu kampuni hii ya simu ilijipanga kusambaza huduma yao nchi
nzima, sambamba na kufungua maduka kwaajili ya kusogeza huduma zetu kwa wateja.
Hali hii imetuongezea wepesi wa utoaji wa huduma zao kwa kufanikiwa kwa kiasi
kikubwa kutambua mahitaji muhimu kwa wateja wetu,
Tanzania imefaidika na uhusiano mzuri uliopo kati yake na Huawei kwa
kuwa na miradi mbalimbali yenye lengo la kuboresha teknolojia ya mawasiliano.
Huawei inampango wa kukuza teknolojia ya mawasiliano nchini Tanzania na sasa imeanza
kushirikiaba kwa karibu na wazawa kama Clara. Milango iko wazi kwa yeyote
anayetaka kutuunga mkono kiabiashara.
Wakati Huawei inazindua duka hilo katika Ukanda wa Kanda ya Ziwa,
Mkurugenzi huyo alitangaza uwepo wa simu mpya ya kisasa, Huawei Y3II na
nyinginezo, katika soko la simu nchini.
Alisema kuwa simu hiyo ina ubora na kuwataka watanzania kutumia,
akifafanua zaidi kuwa ni simu yenye ubora, lakini gharama yake sio kubwa,
ikilinganishwa na simu za makampuni mengine.Pia bidhaa nyingine zitaambatana na
simu hiyo kama matoleo mangine tofauti Huawei P9, Y3c, Y5II ,Y6II, Y3lite na
nyingine nyingi.
Hizi ndizo faida za kuwa na duka kubwa katika Jiji la Mwanza. Kuanzia
sasa wanunuzi wa bidhaa zetu wana fursa ya kupata bidhaa zetu zote kwa wakati. Tunaanza
na simu hii ya Huawei Y3II ambayo kwa hakika kila atakayeamua kuitumia
ataipenda kwa ubora wake.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, Kampuni ya Huawei inaendelea na mchakato
wake wa kusogeza huduma zake kwa wateja wake, kwa lengo la kutimiza malengo
yake ili kupambana na soko la mawasiliano.
Post a Comment