Mkurugenzi
wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Godwin Zacharia (katikati) akimkabidhi kikombe Mpishi
Mkuu wa Bar ya SD Exective ya jijini Mwanza, Mussa Mashauri mara baada ya kuibuka mabingwa katika
mashindano ya Safari Nyama Choma yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.Kulia
ni Meneja wa bia ya Safari Lger, Edith Bebwa.
 |
.
Na Mwandishi
Wetu.Mwanza.
SD EXECUTIVE
Hotel jijini Mwanza wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari
Lager Nyama Choma 2015 yaliyofanyiaka mswishoni mwa wiki katika Uwanja wa Furahisha
na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi milioni moja na Kikombe.
Nafai ya
pili ilichukuliwa Gemestoni Bar ambayo ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi
800,000/=,nafasi ya tatu ni Shooters Bar ambayo ilizawadiwa pesa taslimu
Shilingi 600,000/=,nafasi ya nne ni Lunala ambayoilizawadiwa Shilingi 400,000/=
na nafasi ya tano ni Victoria Prince Bar ambayo ilizawadiwa Shingi 200,000/-
Akizungumza
na wakazi Mwanza walifika katika mashindano hayo, Mkurugenzi wa Benki ya CRDB
Kanda ya Ziwa, Godwin Zacharia kwanza washukuru kampuni ya Bia Tanzania(TBL)
kwa kubuni mashindano hayo ambayo ni mwaka wa nane sasa mfululizo yenye mvuto
wa pekee ambayo yanawapa picha halisi wakazi wa Mwanza kuwa wapi wanaweza
kupata nyama choma bora kutoka katika baa tano ambazo zimeingia fainali katika
jiji la Mwanza.
Alisema Zacharia
kwanza kabisa tunawapongeza kwa kutoa elimu kwa wapishi wa baa mbali mbali za
jijini Mwanza ambayo mliaanza nayo hapo awali tunaamini kwa kupitia hilo wapishi wetu wameelimika si kama
mlivyowakuta na hilo tunawashukuru na tunawaomba muendelee nalo kwani mnaongeza
ajira kwa jamii kama si kupunguza umasikini.
Pili
aliwapongeza baa tano zilizoingia fainali kwani wao ndio baa bora katika baa
zote zinazochoma nyama mkoani humo na aliwaomba waendelee kuilinda hadhi na
sifa hiyo waliyopewa katika jiji la Mwanza na mwisho aliwapongeza mabingwa wapya
SD Exectuve Hoteli kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma kwa
mwaka 2015 na kuwaomba ambao hawakufanikiwa kupata nafasi hiyo wajiandae kwa
mashndano yajayo ya Safari Nyama Choma 2016.
Nae Meneja
wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa aliwapongeza mabingwa wa mwaka 2015, SD
Exective Hoteli na pia aliwashukuru wote walioshiriki toka mchakato ulipoanza
mpaka kufikia kumpata bingwa lakini pia aliwashukuru wakazi wa Mwanza
waliojitokeza kwa wingi kuja kushuhudia nani anatwaa ubingwa wa mashindano ya
Safari Nyama Choma 2015 jijini Mwanza.
Mwisho Edith
aliwaomba washiriki wote ambao walipata zawadi wakatumie vyema zawadi
walizopata kwa kuboresha majiko yao kwa mashindano yajayo ya 2016 lakini pia
wakawe mabalozi wazuri wa bia ya Safari Lager kwenye biashara zao.
|
Post a Comment