Na Mwandishi
Wetu.Arusha.
MILESTONE
PARK Bar jijini Ausha wameibuka mabingwa
katika fainali za mashindano ya Safari Lager Nyama Choma 2015 yaliyofanyiaka
mswishoni mwa wiki katika Nanenane na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi
milioni moja na Kikombe.
Nafasi ya
pili ilichukuliwa Royal Stop Over Bar ambayo ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi
800,000/=,nafasi ya tatu ni Freedom Bar ambayo ilizawadiwa pesa taslimu
Shilingi 600,000/=,nafasi ya nne ni Capital 14 Bar ambayo ilizawadiwa Shilingi
400,000/= na nafasi ya tano ni QX Bar ambayo ilizawadiwa Shingi 200,000/-
Akizungumza
na wakazi jiji la Arusha walifika katika mashindano hayo, Mnadhimu wa Jeshi la
Polisi jijini Arusha, Boniventure Mshongi, kwanza aliwashukuru kampuni ya Bia
Tanzania(TBL) kwa kubuni mashindano hayo ambayo ni mwaka wa nane sasa mfululizo
yamekuwa yenye mvuto wa pekee ambayo yanawapa picha halisi wakazi wa Ausha kuwa
wapi wanaweza kupata nyama choma bora kutoka katika baa tano ambazo zimeingia
fainali katika jiji la Ausha.
Alisema Mshongi
kwanza kabisa tunawapongeza kwa kutoa elimu kwa wapishi wa baa mbalimbali za
jijini Ausha ambayo mliaanza nayo hapo awali tunaamini kwa kupitia hilo wapishi wetu wameelimika si kama
mlivyowakuta na hilo tunawashukuru na tunawaomba muendelee nalo kwani mnaongeza
ajira kwa jamii kama si kupunguza umasikini.
Pili
aliwapongeza baa tano zilizoingia fainali kwani wao ndio baa bora katika baa
zote zinazochoma nyama mkoani humo na aliwaomba waendelee kuilinda hadhi na
sifa hiyo waliyopewa katika jiji la Ausha na mwisho aliwapongeza mabingwa watetezi
ambao wametetea vyema ubingwa wao, Bar ya Milestone Park kwa kutwaa ubingwa wa
mashindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2015 na kuwaomba ambao
hawakufanikiwa kupata nafasi hiyo wajiandae kwa mashndano yajayo ya Safari
Nyama Choma 2016.
Nae Meneja
wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa aliwapongeza mabingwa wa mwaka 2015,Miliestone
Park Bar na pia aliwashukuru wote walioshiriki toka mchakato ulipoanza mpaka
kufikia kumpata bingwa lakini pia aliwashukuru wakazi wa Arusha waliojitokeza
kwa wingi kuja kushuhudia nani anatwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama
Choma 2015 jijini Arusha.
Mwisho Edith
aliwaomba washiriki wote ambao waliopata zawadi wakatumie vyema zawadi
walizopata kwa kuboresha majiko yao kwa mashindano yajayo ya 2016 lakini pia
wakawe mabalozi wazuri wa bia ya Safari Lager kwenye biashara zao.
|
Post a Comment