Meneja wa
bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(wa pili kulia) akimkabidhi kikombe
nahodha wa timu ya klabu ya mchezo wa Pool ya Mpo Afrika, Charles Vernance mara
baada ya kutetea ubingwa wa fainali za mchezo huo ujulikanao kama “Safari
National Pool Competition 2014” ngazi ya
mkoa mkoa wa Temeke uliofanyika Kurasini City Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki.Kulia ni Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga na Kocha wa timu ya
Taifa, Denis Rungu.
Meneja wa
bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(wa pili kulia) akimkabidhi pesa taslimu
Shilingi 800,000/= nahodha wa timu ya klabu ya mchezo wa Pool ya Mpo Afrika,
Charles Vernance mara baada ya kutetea ubingwa wa fainali za mchezo huo
unaojulika kama “Safari National Pool Competition 2014” ngazi ya mkoa mkoa wa
Temeke uliofanyika Kurasini City Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kulia ni
Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga na Kocha wa timu ya Taifa, Denis
Rungu.
Baadhi ya
wachezaji wa Pool wa klabu ya Mpo Afrika na mashabiki wakishangilia na kikombe
mara baada ya kutetea ubingwa wa fainali za mchezo huo unaojulika kama “Safari
National Pool Competition 2014” ngazi ya mkoa mkoa wa Temeke uliofanyika
Kurasini City Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 |
Baadhi ya
wachezaji wa Pool wa klabu ya Delux na mashabiki wakishangilia na kitita cha
pesa taslimu Shilingi 800,000/= mara baada ya kutetea ubingwa wa fainali za
mchezo huo unaojulika kama “Safari National Pool Competition 2014” ngazi ya
mkoa mkoa wa Temeke uliofanyika Kurasini City Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi
Wetu.
FAINALI za
mashindano ya Safari Pool Taifa yajulikanayo kama “Safari National Pool
Competition 2014”, mkoa wa kimichezo wa Temeke jijini Dar es Saalaam na Dodoma
zimefanikiwa kupata mabingwa wa mikoa mwishoni mwa wiki.
Mkoa wa kimichezo
wa Temeke mabingwa ni klabu ya Mpo Afrika walifanikiwa kutetea ubingwa wao wa
mwaka jana wakati mkoani Dodoma Klabu ya Delux ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa
mkoa huo.
Klabu ya Mpo
Afrika na Delux kwa kutwaa ubingwa huo zilizawadiwa pesa taslimu Shilingi
800,000/= kila klabu pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za
kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja wanaume, Temeke; Innocent Sammy alifanikiwa kutwaa ubingwa
na Dodoma ni Regnald Kassimu, ambao
walizawadiwa pesa taslimu Shilingi 400,000/= kila mmoja katika mikoa yao pamoja
na tiketi ya kuwakilisha mikoa yao katika fainali za kitaifa Mkoani Kilimanjaro
kwa mchezaji mmoja mmoja Wanaume.
Upande wa mchezaji
mmoja mmoja Wanawaake,Temeke; Rebeca Magaigwa alitwaa ubingwa na Dodoma ni
Rehema Mussa, ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 300,000/= pamoja na
tiketi ya kuwakilisha mikoa yao katika fainali za kitaifa Mkoani Kilimanjaro
kwa mchezaji mmoja mmoja upande wa Wanawake.
Wiki hii
fainali za Safari Pool Competition 2014,ngazi ya mikoa zinatarajiwa
kuhitimishwa na mikoa ya Morogoro,
Iringa na Mbeya.
Fainali za
kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa kufanyika Septemba
14 mwaka huu, Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni Tabora,Shinyanga,Dodoma
Mbeya,Iringa,Morogoro,Mwanza,Kagera,Manyara,Arusha,Tanga,Pwani,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni
na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.
|
Post a Comment