Mweka hazina
wa Chama cha pool taifa(TAPA), Zaholo Ligalu (kushoto) akimkabidhi nahodha wa
timu ya klabu ya Anatori ya Morogoro pesa taslimu Shilingi 800/000/= mara baada
ya kuibuka mabingwa katika fainali za mchezo wa Pool unajulikana kama “Safari National Pool Competition 2014” ngazi ya mkoa mkoa Mkoa wa Morogoro
uliomalizika mwishoni mwa wiki.
 |
Baadhi ya
wachezaji wa Pool wa klabu ya Anatory ya Morogoro wakishangilia na kitita cha
pesa taslimu Shilingi 800,000/= mara baada ya kutetea ubingwa wa fainali za
mchezo huo unaojulika kama “Safari National Pool Competition 2014” ngazi ya
mkoa mkoa wa Morogoro uliofanyika DDC mjini Morogoro.
Na Mwandishi
Wetu.
KLABU ya Anatory
ya Morogoro,Ngija Masters ya Iringa na Break Point ya Mbeya zimefanikiwa
kutwaa ubingwa wa mikoa katika
fainali za mashindano ya mchezo wa Pool ngazi ya Mikoa yajulikanayo kama
“Safari National Pool Competition 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mikoani
humo na kuzawadiwa kila klabu ferdha taslimu Shilingi 800,000/= pamoja na
tiketi ya kuwakilisha Mkoa kwenye
fainali za Kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.
Kwa matokeo
hayo ya mikoa mitatu ndipo mtanange wa kuwatafuta mabingwa kutoka katika mikoa
17 inayoshiriki fainali za mashindani ya Safari Pool 2014 unafungwa rasmi na
tunaeleza nguvu na masikio kwenye fainali za kitaifa Septemba 14 mwaka huu.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja wanaume Morogoro, Bingwa mtetezi wa mkoa, Mussa Mkwega
alitetea vyema ubingwa wake ,Iringa ni Godlove Chalangwe ndiye alifanikiwa
kutwaa ubingwa wa mkoa wakati Mbeya ni Majaliwa Sipilian alitwaa ubingwa wa
mkoa wa huo na kwa ubingwa huo kila mmoja alizawadiwa pesa taslimu Shilingi 400,000/=
pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa upande wa
mchezaji mmoja mmoja wanaume.
Mchezaji
mmoja mmoja Wanawake waliofanikiwa kutwaa ubingwa ni, Morogoro, Bingwa mtetezi
Rosemary Deus alitetea vyema ubingwa wake, Iringa ni Naomi Ngede alitwaa
ubingwa wakati jijini Mbeya ni Happness Robert ndie altwaa ubingwa wa mkoa na
kwa ushindi huo kala mmoja alizawadiwa pesa taslimu Shilingi 300,000/= pamoja
na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa upande wa mchgezaji
mmoja mmoja wanawake.
Fainali za
kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa kufanyika
Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni
Tabora,Shinyanga,Dodoma Mbeya,Iringa,Morogoro,Mwanza,Kagera,Manyara,Arusha,Tanga,Pwani,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni
na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.
|
Post a Comment