| Wachezaji wa
timu ya klabu ya Mashujaa wakishangilia na kitita cha pesa taslimu Shilingi
800,000/= /= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari
Pool Taifa yaliyofanyika Ilala Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kulia ni Diwani
wa Kata ya Vingunguti, Asaa Simba na Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos
Kafwinga.
Na Mwandishi
Wetu.
FAINALI za
mashindano ya Safari Pool Taifa yajulikanayo kama “Safari National Pool
Competition 2014”, mikoa ya Tabora ,Kagera, Arusha,Kilimanjaro na Mkoa wa kimichezo
wa Ilala zimefanikiwa kupata mabingwa wa mikoa zilizomalizika mwishoni mwa wiki
katika mikoa hiyo.
Mkoa wa
Tabora mabingwa ni Tiptop Pool Klabu,Kagera ni Bilele Pool Klabu,Arusha ni
Ngarenaro Pool Klabu,Kilimanjaro ni Mboya Pool Klabu na Mkoa wa Kimichezo wa
Ilala ni Mashujaa Pool Klabu ambavyo kwa kutwaa ubingwa huo walizawadiwa pesa
taslimu kila klabu Shilingi 800,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mikoa yao
katika fainali za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja wanaume, Tabora ni Omary Hassan, Kagera ni Roberth
Butasigwa, Arusha ni Richard Daudi, Kilimanjaro ni Baraka Jackson na Ilala ni
Yasin Athuman ambao walizawadiwa pesa taslimu Shilingi 400,000/= kila mmoja
katika mikoa yao pamoja na tiketi ya kuwakilisha mikoa yao katika fainali za
kitaifa Mkoani Kilimanjaro.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja Wanawaake, Tabora ni Happiness Morgan, Kagera ni Sajida
Saidi, Arusha ni Merry Gumbo, Kilimanjaro ni Reticia Kileo, na Ilala ni Recho
Kihupi ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 300,000/=.
Fainali za
kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa kufanyika
Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni
Tabora,Shinyanga,Dodoma Mbeya,Iringa,Morogoro,Mwanza,Kagera,Manyara,Arusha,Tanga,Pwani,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni
na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.
|
Post a Comment