WILAYA YA RUNGWE -
WATUHUMIWA 34 WAMEFIKISHWA
MAHAKAMANI TAREHE
25.09.2013 NA JESHI LA
POLISI
KWA KOSA LA KULA NJAMA
NA KUFANYA FUJO/KUFUNGA
BARABARA KUU MBEYA/TUKUYU KWA
MAWE NA MAGOGO.
§
MNAMO TAREHE 25.09.2013
MAJIRA YA SAA 15:35HRS HUKO KATIKA MAHAKAMA
YA WILAYA ILIYOPO - TUKUYU MJINI WILAYA YA RUNGWE
MKOA WA MBEYA. LAURENT S/O NICHOLAUS
KASWAGA, MIAKA 38, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IBURA – KIWIRA NA WENZAKE 33
WALIFIKISHWA KATIKA MAHAKAMA YA
WILAYA NA KUSOMEWA MASHTAKA MAWILI 1.
KULA NJAMA NA 2. KUFANYA FUJO.
AIDHA WATUHUMIWA WALISOMEWA MASHTAKA HAYO NA MWENDESHA MASHTAKA WA POLISI F.3644 D/C JOEL MBELE YA HAKIMU WA MAHAKAMA HIYO MHE.
MEBO MALAKASUKA.
§
KATIKA SHAURI HILO LA JINAI NO. 169/2013 WASHTAKIWA WOTE WAMEPELEKWA GEREZANI AMBAPO UAMUZI WA KUPEWA
AU KUTOPEWA DHAMANA UTATOLEWA NA MAHAKAMA
TAREHE 09.10.2013.
§
AWALI MNAMO
TAREHE 24.09.2013 MAJIRA KATI
YA SAA 18:00HRS HADI SAA
22:00HRS HUKO KATIKA KATA YA KIWIRA VITONGOJI VYA KIBUMBE, MPANDAPANDA, KIWIRA – KATI NA KARASHA
WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. KUNDI
LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI WALIFANYA FUJO KWA KUFUNGA BARABARA KUU YA MBEYA/TUKUYU
WAKITUMIA MAWE MAKUBWA NA MAGOGO ILI MAGARI YASIPITE NA
KUSABABISHA USUMBUFU KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA HIYO. THAMANI HALISI
YA UHARIBIFU ULIOTOKEA BADO
KUFAHAMIKA.
§
HATA HIVYO KATIKA TUKIO HILO GARI T.335 CBE AINA YA
TOYOTA L/CRUISER LIKITOKEA
MBEYA MJINI KUELEKEA TUKUYU LIKIWA LIMEBEBA MIILI YA MAREHEMU WATATU
LILIGONGA MAWE YALIYOKUWA YAMEWEKWA BARABARANI NA WATU HAO KISHA KULIGONGA GARI T. 771 BBE AINA YA TOYOTA
COASTER NA KUSABABISHA MAJERUHI KWA WATU
WAWILI NA UHARIBIFU KWA MAGARI
YOTE MAWILI. CHANZO CHA VURUGU HIZO NI MADAI YA KUONGEZEWA USHURU WA MAZAO [NDIZI] KUTOKA TSHS 100/= ULIOANZA KUTUMIKA MWAKA 1989 NA KUFIKIA TSHS 200/= WAKISHINIKIZA URUDISHWE
USHURU WA ZAMANI NA KUFUATIA VURUGU HIZO JUMLA YA WATUHUMIWA 43
WALIKAMATWA.
§
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA CHANGAMOTO KATIKA JAMII
HAZIWEZI KUTATULIWA KWA KUWEKA MAGOGO NA MAWE BARABARANI BADALA YAKE WATAFUTE
UFUMBUZI KWA KUWASILISHA MATATIZO
KERO NA MAONI YAO KATIKA
MAMLAKA HUSIKA NA KUKAA MEZA
YA MAZUNGUMZO ILI KUPATA UFUMBUZI
KWA KUZINGATIA HOJA.
AIDHA
ANASISISTIZA KUWA KUFUNGA BARABARA KUNALETA MADHARA KWA WATUMIAJI WENGINE WA
BARABARA WAKIWEMO WAGONJWA, WASAFIRI, WAGENI KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI PIA
KUSAFIRISHA MAITI KAMA ILIVYOTOKEA KATIKA GARI T.335 CBE NA KWAMBA JESHI LA
POLISI KAMWE HALITASITA KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA WATU /KIKUNDI CHA WATU
WATAKAOSABABISHA UVUNJIFU WA
AMANI.KWA SASA HALI YA ENEO
HILO NI
|
Post a Comment