WANOKWENDA NIGERIA AIRTEL RISING STARS WATAJWA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza kikosi cha wachezaji
32 wanaosafiri kwenda Lagos, Nigeria wiki ijayo kushiriki mashindano ya
kimataifa kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars.
Afisa
maendeleo wa TFF Salum Madadi amewataja wachezaji wanaounda timu ya
wasichana kuwa ni walinda mlango Najihati Abbasi kutoka mkoa wa kisoka
wa Kinondoni na Niwale Halfan (Temeke). Wengine ni Stumai Abdallah,
Anastazia Anthony, Tatu Iddi (Kinondoni), Vumilia Maharifa, Donisia
Daniel, Maimuna Hamisii na Amina Ally (Ilala).
Aliwataja
wachezaji wengine kuwa ni Shelda Boniphace, Rehema Yahya na Anna
Hebron (Kinondoni), Khadija Hiza (Tanga), Neema Paul, Amina Ramadhani na
Latifa Ahmed (Temeke).
Wanaounda
kikosi cha wavulana ni Arafat Mussa (Ilala) Aziz Hashim (Ilala), Rothan
Mkanwa na Petro Mgaya (Morogoro), Bruno Shayo (Mwanza), Thomas Chideka
(Temeke), George Chota (Morogoro), Luseke Kiggi (Mwanza) na Ramadhani
Kondo (Morogoro).
Wengine
ni Martin Luseke (Mwanza), Omary Hussein (Ilala), Joseph Mushi (Ilala),
Miraj Kwangaya na Salum Issa (Temeke), Optanus Lupekenya (Morogoro) na
Athanas Mdam (Mwanza).
Mashindano
haya ya vijana ya kimataifa yanafanyika kwa mara ya pili mwaka baada ya
yale ya uzinduzi kufanyika jijini Nairobi mwaka jana ambapo Tanzania
iliwakilishwa na timu ya wavulana pekee ambayo hata hivyo ilitolewa
katika hatua za awali huku timu ya Niger ikitawazwa kuwa mabingwa.
Airtel
imeanzisha mashindano haya ya vijana barani Afrika kwa nia ya kusaidia
upatikanaji wa vijana wenye vipaji vya soka kuanzia ngazi ya chini
kabisa hadi ngazi ya Taifa. Airtel Rising Stars inatoa fursa kwa vijana
kudhihirisha uwezo wao kwa makocha wa Taifa na kimataifa na kuweza
kujiendeleza zaidi kisoka.
Hivi
sasa Airtel Rising Stars ni moja ya matukio muhimu ya kisoka kwenye
kalenda ya Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF). Huanzia katika
hatua ya usajili ikifuatiwa na mechi za mtoano ili kupata wachezaji
nyota wa kuunda timu za mikoa ambazo huchuana katika ngazi ya Taifa.
Post a Comment