TAMASHA LA JAMBO FESTIVAL KUKUTANISHA WASHIRIKI ZAIDI YA 100.
ZAIDI ya washiriki 100 kutoka ndani na nje ya nchi watashiriki
kwenye tamasha la Sanaa na utamaduni la Jambo Festival litakalofanyika oktoba
23 hadi 27 mwaka huu katika viwanja vya Suye vilivyopo mjini hapa.
Mwenyekiti wa tamasha hilo, la Jambo Festival 2013 ,Augustine Namfua alisema kuwa , tamasha hilo ni la pili kufanyika mkoani Arusha ambapo wamekuwa wakifanya kila mwaka lengo likiwa ni kuwawezesha washiriki mbalimbali kuweza kuonyesha bidhaa zao za kitamaduni kutoka ndani na nje ya nchi.
Alisema kuwa, tamasha hilo ambalo ni la kimataifa pia litawashirikisha washiriki kutoka nchi za Ufaransa,na Angentina ambao wataweza kuonyesha matamasha mbalimbali ya kitamaduni sambamba na kuonyesha bidhaa zao za kitamaduni .
Alisema kuwa, tamasha hilo litaenda sambamba na matukio mbalimbali ya kiasili ikiwemo maonyesho ya mavazi ya kiasili,pamoja na tamasha la kiasili kutoka vikundi jijini Tanga, Arusha, na Dar es Saalamu .
Namfua aliongeza kuwa, pia
kutakuwepo na tamasha la muziki wa kisasa pamoja na onyesho
la mavazi , na ubunifu wa mavazi ambapo katika tamasha hilo kwa
siku hizo kila siku kutakuwa na matamasha mbalimbali ambayo yatakuwa yakionyeshwa
.
Aliongeza kuwa, tamasha hilo limekamilika kwa asilimia 50 huku watu mbalimbali wakiwemo binafsi, mashirika na taasisi mbalimbali zinazohusika na maswala ya sanaa na tamaduni wanaendelea kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kushiriki katika tamasha hilo .
‘tamasha la mwaka jana lilifana sana kwani tuliweza kupata washiriki wengi sana kutoka ndani na nje ya nchi na lilikuwa na mwitiko mkubwa sana , huku watu mbalimbali wakipata fursa ya kuonyesha sanaa zao na tamaduni mbalimbali na kuweza kujifunza kutoka kwa wenzetu wan je ya nchi ndio maana tumeamua kufanya tena mwaka huu mwezi wa kumi hivyo tunatarajia watu mbalimbali kushiriki kikamilifu katika tamasha hilo’alisema Namfua.
Aidha aliwataka watu mbalimbali kufika katika tamasha hilo na kuonyesha bidhaa zao za kitamaduni zinazotengenezwa kwa mikono pamoja na kutangaza tamaduni zao za kiafrika , huku akiwataka wadau mbalimbali kuonyesha moyo katika kusaidia matamasha hayo ili yaendelee kufanyika mara kwa mara.
Post a Comment