MAONYESHO YA WANASAYANSI VIJANA WA SHULE ZA SEKONDARI TANZANIA FROM MAE
Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Jangwani Liberata Kasekwa (kushoto) akimulezea mwl. Salome Mbago kutoka shule ya sekondari Morogoro (katikati)
aliyeshikilia chupa nyenye dawa ya kuulia wadudu iliyotengenezwa kwa
kutumia limao kwenye maonesho ya Wanasayansi Vijana wa Tanzania
yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo jijini Dar es
Salaam. Picha na Eleuteri Mangi - MAELEZO
Mwamuzi wa maonesho ya Wanasayansi Vijana wa Tanzania kutoka Kitengo cha Masuala ya Teknolojia wa ESB International Edwina O’ Callaghan (kushoto) akisikiliza maelezo juu ya matumizi ya umeme wa mwanga wa jua kwa matumizi ya kupikia kwa kutumia jiko lililotengenezwa kwa ajili ya kupikia (Oven) kutoka kwa mwanafunzi Deogratius Daudi wa shule ya Sekondari Mwembeni kutoka mkoani Mara (kulia), katikati ni mwanafunzi Yusuph Tito.
Mbilimbi
ni tunda linalotumika kama chachandu (kiungo cha mboga) kwa ajili ya
kuongeza ladha ya chakula, lina uwingi wa asidi (citric acid) ambayo ni
muhimu kwa binadam mahususi kwa ajili ya mmeng’enyo wa chakula mwilini.
Linatumiwa hasa mikoa ya ukanda wa Pwani ikiwemo Dar es Salaam,
Morogoro,Pwani, Lindi na Tanga. Shule ya Sekondari ya Wasichana Kilakala
kutoka mkoani Morogoro (imewakilishwa na Irene Maigwa na Betha Shao
wote kidato cha sita) kwenye banda lao la maonesho ya Wanasayansi
Vijana wa Tanzania yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo
jijini Dar es Salaam.
Post a Comment