ad

ad

VILABU SABA VYATINGA FAINALI SAFARI POOL 2013.

 Meneja Matukio( TBL) kanda ya ziwa Erick Mwayela (wa pili kulia) akikabidhi zawadi ya fedha tathilimu shilingi 700000/=  nahodha wa klabu ya Pasiansi mara baada ya kuibuka Mabigwa wa mashindano ya Safari Lager National Pool Competition 2013 Mkoa wa Mwanza.Katikati ni Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa Pool Mkoa wa Mwanza , Michael George kushoto ni Mratibu wa mashindano hayo Alfani.

Na Mwandishi Wetu.

FAINALI za mashindano ya mchezo wa Pool Taifa ngazi ya Mkoa yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia nchini(TBL) kupitia Bia ya Safari Lager yamemalizika vyema kwa kupata vilabu vitakavyowakilisha mikoa katika mikoa sita ambayo ni Tanga,Morogoro,Arusha,Manyara,Mwanza na Mkoa wa Pwani

Mkoa wa Tanga Klabu Bingwa iliyoibuka  2013 ni Spider,na kwa ubingwa huo walizawadia fedha taslimu shilingi 700,000/= na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Taanga kwenye fainali za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Morogoro mwezi ujao

Upande wa wachezaji mmoja mmoja(Singles) wanaume,Jemes Msemo alitwaa ubingwa,hivyo kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 350,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa kwenye fainali za kitaifa Mkoani Morogoro.

Mkoa waMorogoro, Klabu ya Anatori  imefanikiwa kutetea ubingwa wa Mashindano  hivyo kujinyakulia zawadi ya fedha taslimu shilingi 700,000/=  na  pamoja na  tiketi ya kuwakilisha Mkoa kwenye  fainali za kitaifa ambapo mwaka huu wa 2013 Mkoa wa Morogoro watakuwa wenyeji wa mashindano hayo.

 
Katika mchezo wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) wanaume mchezaji, Mussa Mkwenga  alifanikiwa kutwaa ubingwa  na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 350,000  na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa.


Upande wa wanawake mchezaji, Rosemary Deus alitwaa ubingwa na kuzawadiwa shilingi 250,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa Mkoani hapo.


Mkoa wa Arusha,Klabu ya Ngarenaro ilitwaa ubingwa na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 700,000 na tiketi ya kuwakilisha Mkoa kwenyefainali za kitaifa.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume,Nuru Andrew alitwaa ubingwa na kuzawadiwa shilingi 350,000 na tiketi ya kuwakilisha Mkoa kwenye fainali za kitaifa na Upande wa wanawake mmoja mmoja Sofia Shabani alitwaa ubingwa na kuzawadiwa 250,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa.

Mkoa wa Manyara,Klabu ya SuperSport  wameliibuka mabingwa na kuzawadiwa shilingi 700,000 pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa wakati  upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume,Paul Gagaa alitwaa ubingwa na kuzawadiwa shilingi 350,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa wakati upande wa kinadada,Ashura Juma alitwaa ubingwa na kuzawadiwa shilingi 250,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa Mkoani Morogoro.

Mkoa wa Mwanza, Klabu ya Paseansi  wameliibuka mabingwa na kuzawadiwa shilingi 700,000 pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa wakati  upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume,Fidelis Salaba alitwaa ubingwa na kuzawadiwa shilingi 350,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa wakati upande wa kinadada, Rukia Issa alitwaa ubingwa na kuzawadiwa shilingi 250,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa .

Mkoa wa Pwani, Klabu ya Yakwetu  wameliibuka mabingwa na kuzawadiwa shilingi 700,000 pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa wakati  upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume,Augustino Kasuka alitwaa ubingwa na kuzawadiwa shilingi 350,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa wakati upande wa kinadada, Shamira Othman alitwaa ubingwa na kuzawadiwa shilingi 250,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa .

Mkoa wa Lindi, Klabu ya Paseansi  wameliibuka mabingwa na kuzawadiwa shilingi 700,000 pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa wakati  upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume,Fidelis Salaba alitwaa ubingwa na kuzawadiwa shilingi 350,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa wakati upande wa kinadada, Rukia Issa alitwaa ubingwa na kuzawadiwa shilingi 250,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa .

No comments