SUPER D KUFANYA ZIARA YA KUHAMASISHA MCHEZO WA NGUMI MIKOA 16
SUPER D AKIWA NA VIFAA VYAKE VYA KUFUNDISHIA MASUMBWI |
KOCHA wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' yupo katika ziara ya kutembelea mikoa mbalimbali hapa nchini tangia mwishoni mwa mwezi uliopita ambapo mpaka sasa katika ziara yake hiyo kesha tembelea mikoa kadhaa ya Tanzania Bara akianzia na Tanga,Moshi,,Arusha,Karatu,Babati Mwanza ,Shinyanga na Kahama
Ziara hiyo yenye lengo la kuhamasisha mchezo wa ngumi kwa vijana na kuwapa mbinu mpya baadhi ya makocha wa mikoa husika ili mchezo wa ngumi uweze kusonga mbele ingawa mchezo huo unapendwa na wenga na kukwepwa na wadhamini ndicho kitu kinachokifanya mchezo wa masumbwi uonekane umeshuka hadhi yake wakati bado upo juu
SUPER D akiwa MWANZA |
Post a Comment