ad

ad

USIKU WA BI KIDUDE WAJA

bi kidude kuenziwa ziff,
usiku wa bikidude,
usiku wa wanawake ziff,
jukwaa la wanawake
 
Na Andrew Chale, Zanzibar
 
WANAMUZIKI Nguli nchini wakiongozwa na  Sit bin Saad ambaye ni mjukuu wa marehemu Bi.Kidude,Synerg,Baby J wote hawa ni kutoka Zanzibar  Linah na THT Band kutoka Dar es Salaam kesho watawasha moto ndani ya mabo klabu kwa ajili ya  kumuenzi marehemu Bi.Kidude ambaye aliwahi kutumbuiza katika matamasha ya ZIFF yaliyowahi kufanyika.
 
 
Tamasha la filamu la nchi za Jahazi maarufu kama ZIFF linaendelea kupamba moto na kesho ni usiku maalumu wa wanawake katika kumuenzi  marehemu Bi.Kidude katika tamasha hilo.
 
Tamasha hilo ambalo lina siku ya 5 tangu kuanza kwake limekuwa ni kivutio kikubwa kwa wakazi na wageni kutoka kila kona ya dunia  kuwapa burudani kulingana na mahitaji.
 
Usiku  wa wanawake unatarajia kufanyika jioni ya leo ndani ya Mambo klabu ampapo wasanii watakao tumbuiza katika tamasha hio watakuwa ni wanawake pekee  ambapo  mjukuu wa marehemu Bi.KIdude atafungua dimba kutoa  burudani hiyo.
 
Wanawake wameombwa kuhudhuria kwa wingi kwakuwa  tamasha la siku ya leo ni kwa ajili ya wanawake.
 
 katika tamasha hilo la usiku wa wanawake wasanii hao wataweza kukonga nyoyo za mashabiki wake na kufanya kufana kwa tamasha hilo ambalo linamkumbuka Bi.kidude kwa mchango wake ambao alikuwa akiutoa katika kipindi chake chote cha uhai wake.
 
Hata hivyo burudani hiyo itaambatana na kuonyeshwa kwa filamu mbili tofauti ikiwemo ya The Last Fishing Boat kutoka Malawi na Lilet never Happened kutoka Netherland.

TBL YASAIDIA MIRADI YA MAJI YA SH. MIL 50 CHUO KIKUU CHA ST AUGUSTINE, SH. MIL. 49 MISUNGWI, MWANZA

 Meneja Mauzo wa Na Usambazaji wa TBL Kanda ya Ziwa, Malaki Staki wa kwanza (kulia), kushoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino, Dkt,Charles Kitima, kwa pamoja wakitaka utepe kuzindua moja ya matanki ya kuhifadhi maji,katika chuohicho.Mradi huo umetekelezwa na TBL kwa gharama y ash. Milioni 50.
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Dkt Charles Kitima kushoto akimshukuru  Meneja Mauzo na Usambazaji wa TBL Kanda ya Ziwa, Malaki Staki, muda mfupi baada ya kuzindua mradi wa matanki ya kihifadhi maji chuoni hapo jana.Mradi huo wa ujenzi wa mantaki hayo mawili yenye ujazo wa lita 100,000 kila kila mmoja umegharimu sh. Milioni 50.

 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, Dkt Charles Kitima wa nne kutoka kushoto, Meneja Mauzo na Usambazaji wa TBL Kanda ya Ziwa, Malaki Staki, wa nne  kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhi matanki mawili ya maji kwa chuo hicho.Wa pili kutoka kulia ni Askafu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, Askofu Yuda Thadeus  Ruwa’ich.wa kwanza , kulia ni  Askofu Paul Luzoka .kulia kwa Dkt Kitima ni Padri Mwanjonde.

 Mkurugenzi wa Uhusiano na  Sheria wa TBL, Stephen Kilindo,akizungumza na baadhi ya  wenyeviti  (hapo pichani) wa Vijiji vya Wilaya ya Misungwi ()muda mfupi kabla ya kukabidhi hundi ya sh.49 milioni kwa ajili ya kukarabati visima vya maji wilayani humo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya hiyo, Nathan Mshana  na Meneja Mauzo na Usambazaji TBL Kanda ya Ziwa, Malaki Staki.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi, Nathan Mshana akizungumza na baadhi ya  wenyeviti wa vijiji  wilayani humo (hawapo pichani), muda mfupi kabla ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni 49 kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)
  Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ziwa.Malaki Staki akimkabidhi mfano wa hundi Mkurugenzi wa Ufundi wa kampuni ya Nyagama Investment Ltd  Simon Mazuka, kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ukarabati wa visima 20 vya maji katika baadhi ya vijiji vya wilaya ya Misungwi.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Stephen Kilindo,wa pili ni kutoka kushoto ni Mhandisi wa Maji Wilayani Misungwi,Jumanne Kitiku.Nyuma ya Malaki ni DED wa Halmashauri ya Misungwi, Nathan Mshana na wa kwanza kushoto ni Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo,Pastory Mkaruka.
Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ziwa Malaki Staki ,akiwa katika picha ya pamoja na wenyeviti wa baadhi ya vijiji vya wilaya ya Misungwi ambao mradi ya ukarabati wa visima utakaoanza kutekelezwa mapema mwezi huu,  baada ya Kampuni ya TBL kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 49.

No comments