ad

ad

BREAKING NEWS: MOYES ASEMA: ROONEY HAUZWI, ATAENDELEA KUWA MCHEZA WA UNITED - KUHUSU RONALDO ASHINDWA KUKATAA WALA KUKUBALI KUTAKA KUMSAJILI


Kocha wa Manchester United David Moyes leo hii amethibitisha kwamba mshambuliaji wa klabu hiyo Wayne Rooney hayupo sokoni na ataendelea kuicheza klabu hiyo kwa mingi ijayo.

Akizungumza kwenye mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu ajiunge na klabu hiyo akichukua nafasi ya Sir Alex Ferguson, Moyes alisema: "Nimeongea na Wayne Rooney. Wayne yupo nyuma ya mabao 40 kumfikia Sir Bobby na Denis Law. Wayne hauzwi - ni mchezaji wa Manchester United - na ataendelea kubakia kuwa mchezaji wa Manchester United. Nimekuwa na mikutano nae kadhaa. Amerudi kwenye hali nzuri na anafanya vizuri mazoezini. Tunajaribu kufanya kila kitu kumrudisha Wayne Rooney kuwa kama alivyokuwa zamani - Wayne Rooney ambaye tunamjua.

"Vyovyote vilivyotokea kabla, tunafanya kazi pamoja sasa. Macho yake yanaonyesha ni mtu mwenye furaha, ni lazima niseme Wayne hauzwi. Kuliwahi kuwepo mkutano wa siri baina ya Rooney na Sir Alex. Mie naendelea mbele sasa, sijui nini kilizungumzwa kwenye mkutano huo. Ninachofikiria sasa ni kusonga mbele na kufanya kazi ya kumrudisha Wayne Rooney kwenye ubora wake. "
Alipoulizwa kuhusu Cristiano Ronaldo, Moyes alijibu: "Sitomzungumzia yeye moja kwa moja na wachezaji wengine wa vilabu vingine. Lakini hii klabu siku zote imekuwa ikivutiwa na wachezaji bora duniani."
Pia Moyes alithibitisha kwamba winga mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa kutoka Crystal Palace - Wilfred Zaha ambaye amekuwa akiwindwa na vilabu vingi kujiunga navyo kwa mkopo - Moyes amesema mchezaji huyo ataungana na Manchester United kwenye tour ya pre-season, kama ilivyo kwa wachezaji wengine. 
Wakati huo huo alipoulizwa kuhusu usajili wa wachezaji wapya, Moyes amesema angependa kusajili wachezaji mapema lakini mambo yamekuwa yakichelewa kutokana na makocha ambao ndio wanaothibitisha uuzwaji wa wachezaji wengi wamekuwa likizo au ndio wanaingia kwenye vilabu vyao vipya.
Chanzo: Shaffih Dauda Blog

VIONGOZI MBALIMBALI WALIOTEMBELEA BANDA LA TTCL KATIKA MAONYESHO YA KIBIASHARA YA 37 YA KIMATAIFA JIJINI DAR

IMG_0095Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akimsikiliza Afisa Biashara wa Mkongo wa Taifa Bw. Thomas Lemunge wakati alipotembelea banda hilo. IMG_0039 Baadhi ya wafanyakazi wa TTCL wakati wa Ufunguzi rasmi wa maonesho ya 37 .
IMG_9272 (2)Mfalme Mswati III na Waziri Mkuu mhe. Mizengo Pinda wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Idara ya Huduma na Bidhaa zitolewazo na TTCL Bw. Ernest Isaya wakati walipotembelea katika banda hilo. IMG_0081Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe. Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni baada ya kupata maelezo ya kina kuhusu Mkongo wa Taifa unavyosaidia kurahisisha biashara kwa njia ya mtandao, elimu-mtandao, matibabu-mtandao pamoja na kuunganisha n.k
IMG_0103wateja wakipata maelezo kuhusu huduma ya ziada wanazoweza kupata kupitia simu za mkononi za TTCL ikiwa ni pamoja na huduma ya ‘teleconference’ ambapo mteja ana uwezo wa kuongea na watu zaidi ya watano kwa wakati mmoja ( kufanya mkutano kwa njia ya simu )n.k.
IMG_0105wateja wakipata maelezo kuhusu huduma ya ziada wanazoweza kupata kupitia simu za mkononi za TTCL ikiwa ni pamoja na huduma ya ‘teleconference’ ambapo mteja ana uwezo wa kuongea na watu zaidi ya watano kwa wakati mmoja ( kufanya mkutano kwa njia ya simu )n.k.
IMG_0192 
Banda la kampuni ya simu ya TTCL kwenye viwanja wa vya maonyesho ya biashara ya TANTRADE.

No comments