Umoja wa Mataifa yanyakua Tuzo Maalum katika Maonyesho ya 37 ya Biasharaya Kimataifa jijini Dar
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la
Shirika la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya 37 ya Biashara ya
Kimataifa yaliyofikia tamati jana kwenye viwanja vya Mwl. Julius Nyerere
jijini Dar. Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara
Dk. Abdallah Kigoda pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini
Dk. Alberic Kacou.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ( wa pili
kushoto) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Wajasiriamali
wanaofadhiliwa na UNIDO kwenye banda la Shirika la Umoja wa Mataifa
akiwa ameambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda
(kushoto) pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic
Kacou (wa pili kulia) wakati wa sherehe za kufunga Maonesho ya 37 ya
Biashara ya Kimataifa jijini kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Tuzo
maalum waliyokabidhiwa shirika la Umoja wa Mataifa nchini kwa kutambua
mchango wao wa kuhamasisha Jamii (UN Special recognition for community
awareness) wakati wa sherehe za kufunga Maonesho ya 37 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Post a Comment